Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wapinzani Sudan waandamana  kutaka utawala wa kijeshi
Kimataifa

Wapinzani Sudan waandamana  kutaka utawala wa kijeshi

Maandamano ya wapinzani Sudan
Spread the love

 

WAKATI mataifa mengi duniani yakikwepa utawala wa kijeshi, kwa upande wa Sudan baadhi ya wananchi wameandamana kupinga Serikali ya mseto inayoundwa na viongozi wa kawaida wa kisiasa na wale wa jeshi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wapinzani hao wa serikali ya mpito ya Sudan waliandamana katika barabara za mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum juzi tarehe 17 Oktoba wakishinikiza jeshi pekee kudhibiti nchi hiyo.

Maelfu ya watu kadhaa walikusanyika nje ya ikulu ya rais huku mgogoro wa kisiasa ukiendelea kuongezeka.

Jeshi na makundi ya kiraia yamekuwa yakigawana madaraka tangu Rais Omar al-Bashir alipong’olewa madarakani mwaka 2019.

Tangu wakati huo, viongozi wa jeshi wamekuwa wakidai mageuzi ya Umoja wa Vikosi vya Uhuru na Mabadiliko (FFC), muungano wa raia ambao uliongoza maandamano ya kumpinga Bashir na kuunda sehemu muhimu ya serikali ya mpito.

Vikosi vya wanajeshi pia vimetaka kubadilishwa kwa baraza la mawaziri.

Hata hivyo, viongozi wa raia wanasema kuwa madai hayo ni njama ya kutaka kunyakua mamlaka kutoka kwa wanajeshi.

“Tunahitaji serikali ya kijeshi, serikali ya sasa imeshindwa kutuletea haki na usawa,” mwandamanaji mmoja aliiambia AFP.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!