December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Vick Kamata afichua mateso ubunge miaka mitano iliyopita

Vick Kamata

Spread the love

 

ALIYEKUWA mbunge wa Viti Maalum, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Vick Kamata Servacius Likwelile, ameibuka na kueleza mambo mazito ambayo yeye na baadhi ya wabunge wenzake, waliyapitia katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa Rais John Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akiandika katika ukurasa wake Instagram, Vick amesema, “miaka mitano iliyoisha 2020, niliishi maisha magumu bungeni.” Anamtaja mwenzake ambaye anadai kuwa ubunge ulimtokea puani kama yeye, ni Dk. Dalali Peter Kafumu, ambaye alikuwa mbunge wa Igunga, mkoani Tabora.

Vick ameeleza hayo, muda mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Arusha, kumhukumu kifungo cha miaka 30 gerezani, Lengai ole Sabaya, ambaye alikuwa mkuu wa wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro.

Kwa habari zaidi, soma gazeti lako la Raia Mwema, toleo la leo Jumatatu, 18 Oktoba 2021.

error: Content is protected !!