Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mabilioni yamwaga ujenzi wa miradi ya maji
Habari za Siasa

Mabilioni yamwaga ujenzi wa miradi ya maji

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
Spread the love

 

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso, amesema katika kipindi cha miezi sita cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, Serikali yake imetoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji nchi nzima, hasa katika maeneo yenye ukame. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Aweso ameyasema hayo leo Jumatatu, tarehe 18 Oktoba 2021, katika uzinduzi wa mradi wa maji Longido mkoani Arusha.

“Katika wizara yetu ya maji kwa muda wa miezi sita ambayo umekaa madarakani, bajeti yetu ilikuwa Sh. 600 bilioni, lakini kutokana na changamoto ya maji rais umetuongezea Sh. 207 bilioni. Tunakwenda sasa Sh. 800 bilioni, umetupa uwezo wa fedha hizo haijawahi tokea,” amesema Aweso.

Aweso amesema, kutokana na ongezeko la bajeti ya wizara hiyo, miradi ya maji takribani 1,176 inatarajiwa kujengwa maeneo ya vijijini.

Amesema, Serikali imetoa Sh. 139 bilioni kwa ajili ya utekelezaji miradi ya maji, ambapo Sh. 38 zitanunua vifaa ikiwemo magari ya kuchimba visima 25, huku Sh. 101 bilioni ikitarajiwa kujenga miradi ya mfano nchi nzima.

Aidha, Aweso amesema, wizara hiyo imepata fedha kiasi cha Dola za Marekani 500 milioni kutoka nchini India, ambazo zitajenga miradi ya maji kwenye miji 28.

“Kutokana na mahusiano yako mazuri na maeneo mengi ya mataifa, sisi tumepata fedha dola 500 milioni kwa ajili ya kutatua tatizo la maji nchini, tunakwenda kutekeleza miradi ya maji katika miji 28. Tumeshapata wakandarasi, tuanomba kibali waende site wabunge wanategemea huu mradi,” amesema Aweso.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

error: Content is protected !!