Thursday , 16 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the love

MWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge mkono chama chake cha zamani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika Uchaguzi Mkuu wa 2025 na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Dk. Slaa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, ametoa wito huo leo Jumatatu, akizungumza kwa njia ya simu katika mkutano wa hadhara wa Makamu mwenyekiti wa chama hicho bara, Tundu Lissu, uliofanyika jijini Dodoma.

Mwanasiasa huyo amesema, Chadema ndiyo chama pekee cha upinzani kinachoonyesha dhamira ya kutatua matatizo yanayowakabili wananchi.

“Ninawaomba watanzania tuhakikisheni tunaungana na Chadema, tunawaondoa hawa ambao sasa hivi wameonesha nia ya uhakika kwamba hawako upande wa wananchi. Mfano mjamzito anaenda hospitali lazima alipie gharama, huyu mama analeta mtanzania mpya anaongeza idadi yetu kweli tunashindwa kumlipia? Mbona Rais anapanda ndege kila siku ana hela za kutosha?” amesema Dk. Slaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Mbunge Mwakasaka alitaka Jeshi la Polisi kutenda haki

Spread the loveEMMANUEL Adamson Mwakasaka, Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), amelitaka Jeshi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia ateua wenyeviti wa taasisi mbalimbali

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amefanya uteuzi wa viongozi...

Habari za SiasaTangulizi

Madeleka aibwaga Jamhuri kesi za kubambikiwa

Spread the loveWakili Peter Madeleka ameshinda rufaa yake namba 263 ya mwaka...

Habari za SiasaTangulizi

Sheikh Ponda ataka kura ya maoni kuamua hatma ya muungano

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa...

error: Content is protected !!