Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa
Spread the love

WIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka wa fedha wa 2024/25 kiasi cha Sh. 2.72 trilioni, ikiwa ni ongezeko kutoka bajeti ya Sh. 2.08 trilioni iliyopitishwa 2023/24. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti hiyo, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amesema Sh. 2.61 trilioni zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo na Sh. 114.74 bilioni kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

“Fedha za matumizi yakKawaida zilizotengwa zinajumuisha Sh. 86.66 bilioni kwa ajili ya mishahara ya watumishi na Sh. 28.08 bilioni kwa ajili ya matumizi mengineyo. Vilevile, fedha za miradi ya maendeleo zilizotengwa zinajumuisha Sh. 2.52 trilioni ni fedha za ndani na Sh. 90.56 bilioni ni fedha za nje,” amesema Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa ametaja miradi ya maendeleo iliyopewa kipaumbele katika bajeti ijayo ni ujenzi wa viwanja vya ndege, uboreshaji wa usalama wa usafiri katika Ziwa Victoria, Bandari ya Dar es Salaam, ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), ukarabati wa Reli ya Tazara na mradi wa uboreshaji Kampuni ya NdegeTanzania (ATCL).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!