SERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184 za ngazi ya halmashauri, ili kuhakikisha inasogeza karibu huduma za bora za afya kwa wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa…(endelea).
Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 6 Mei 2024, katika Hospitali ya Wilaya ya Iringa Mjini (Frelimo), mkoani Iringa.
Akizungumza wakati anazindua mpango huo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, amesema zoezi hilo litaenda sambamba na usambazaji wa madaktari bingwa waliopewa jina la madaktari wa Rais Samia Suluhu Hassan, katika hospitali husika ili kuwapa uzoefu watoa huduma wake.
“Tumewaletea jopo nzuri sana la madaktari bingwa wa Rais Samia ili kuleta huduma za kibingwa na bobezi karibu na wananchi na azma kubwa ni kuboresha huduma za afya nchini,” amesema Ummy.
Ummy amesema lengo la madaktari bingwa hao kusambazwa katika hospitali za halmashauriu ni kuwajengea uwezo watoa huduma katika maeneo yao ya kazi ili kuimarisha utambuzi wa magonjwa, matibabu ya wagonjwa, upasuaji pamoja na rufaa kwa wagonjwa wa ngazi ya hospitali ya halmashauri.
Leave a comment