Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Biashara Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati
BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Reli ya kisasa ya SGR
Spread the love

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha usimamizi katika miradi ya maendeleo ya kimkakati ya uchukuzi ikiwemo barabara na reli, ili kuhakikisha inatekelezwa kwa ufanisi na thamani ya fedha iwepo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Wito wa kamati hiyo umetolewa bungeni jijini Dodoma leo Jumatatu na mwenyekiti wake, Seleman Kakoso, akiwasilisha maoni ya kamati yake kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Uchukuzi, kwa mwaka wa fedha wa 2024/25.

Aidha, Kakoso amesema kamati hiyo inaishauri serikali kuongeza ubunifu katika ukusanyaji mapato yatokanayo na miradi ya uchukuzi, ili yaongezeke.

“Kamati imeshuhudia kwa sehemu kubwa miradi ya kimkakati ambayo ilianza kutekelezwa katika serikali ya awamu ya tano, serikali ya awamu ya sita imetekelezwa kwa ufanisi. Kwa mkuktadha huo na kwa kuthamini mtaji wa fedha za maendeleo zinatokana na kodi za wananchi, kamati inaishauri serikali kuongeza ufanisi na ubunifu katika utekelezaji wa miradi hiyo,” amesema Kakoso na kuongeza:

“Tunaishauri Serikali kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi yake yote ili iweze kuakisi viwango bora endelevu na kuwepo kwa thamani ya fedha.”

Miongoni mwa miradi ya mkakati ya miundombinu ambayo ilianza kutekelezwa katika Serikali ya Awamu ya Tano na kuendelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita, ni ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na miradi ya barabara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Sloti ya Wild 81 malipo kwa njia 81 Meridianbet kasino

Spread the love Meridianbet kuna mchezo wa sloti wa kusisimua sanaambao utakufurahisha....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

error: Content is protected !!