Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the love

SERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi 11 katika Bandari ya Dar es Salaam, ili kuongeza tija na ufanisi katika utendaji wa bandari hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 6 Mei 2024 na Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2024/25, bungeni jijini Dodoma.

Mwekezaji huyo mpya anatafutwa bandarini, baada ya Serikali kusaini mkataba mwingine wa ushirikiano wa uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam, kampuni ya Dubai Wolrd Port (DP World) kutoka Dubai, ambayo itaendesha gati namba nne hadi saba.

“Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imeendelea kushirikisha sekta binafsi katika uendeshaji bandari kwa baadhi ya maeneo kwa kuingia ubia na kampuni binafsi katika kuendeleza na kuendesha shughuli za bandari kuanzia gati namba nne hadi saba,” amesema Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amesema “kwa sasa hatua mbalimbali zikiwemo za makabidhiano na mobilization zinaendelea ili kuruhusu utekelezaji rasmi kuanza. Aidha, Serikali inaendelea na taratibu za kumpata Mwekezaji mwingine atakayekuwa na jukumu la kufanya shughuli za uendeshaji kuanzia Gati Namba 8 hadi 11. Lengo ni kuongeza tija katika utendaji wa bandari.”

Katika hatua nyingine, Prof. Mbarawa amesema shughuli za uendeshaji bandari nchini zinazosimamiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania  (TPA) zimeongezeka, ambapo shehena za mizigo zimeongezeka kutoka tani 14.56 milioni zilizohudumiwa 2022/23 hadi kufikia tani 20.72 milioni zilizohudumiwa 2023/2024.

“ Ongezeko hilo ni sawa na la asilimia 42.31. Aidha, kwa upande wa makasha, TPA ilihudumia makasha 805,167 ikilinganishwa na makasha 688,609 katika kipindi kama hicho mwaka 2022/23, sawa na ongezeko la asilimia 16.92. Ongezeko hilo la shehena ya mizigo na makasha limetokana na mikakati mbalimbali inayoendelea kutekelezwa ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa Bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara,” amesema Prof. Mbarawa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile aukwaa uenyekiti wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!