Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo
KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the love

Rais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu kuanzia kesho Ijumaa kutokana na kifo cha Mkuu wa Majeshi nchini hiyo CDF- Francis Ogolla. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

CDF Ogolla amefariki dunia leo Alhamis katika ajali ya helkopta ya jeshi la nchi hiyo iliyoanguka na kushika moto katika eneo la Sindar, lokesheni ya Kaben kwenye mpaka wa kaunti ya Elgeyo Marakwet na Pokot Magharibi nchini humo.

Ndege hiyo iliyokuwa na watu nane, watano wamefariki dunia papo hapo akiwamo mkuu huyo wa majeshi huku wengine watatu wakiripotiwa kupata majeraha.

Akihutubia  taifa la Kenya leo jioni Rais Ruto amesema maomboleza hayo yataanza kesho tarehe 19 Aprili ikiwa ni pamoja na bendera kupepea nusu mlingoti.

Awali Kamanda wa Kaunti, Peter Mulinge alisema ndege hiyo ilianguka muda wa saa 8:50 mchana.

Ndege hiyo ilikuwa miongoni mwa zingine tatu na ilikuwa inaondoka eneo la Cheptulel Pokot Magharibi na ilikuwa ya kwanza kupaa, kabla ya kuanguka dakika chache baadaye.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

Habari za SiasaTangulizi

Wizara Katiba na Sheria yaliomba Bunge Sh. 441.2 bilioni

Spread the love  WIZARA ya Katiba na Sheria imeliomba Bunge liidhinishe bajeti...

error: Content is protected !!