Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Biashara NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika
BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the love

Ubunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na uwekezaji wenye tija inaoufanya kuwahudumia wateja kwa ufanisi vimekuwa kivutio kikubwa kwenye mkutano wa wakaguzi wa ndani wa Afrika unaofikia tamati leo Alhamis jijini Arusha. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

 Wafanyakazi kwenye banda la benki hiyo katika viwanja vya Ukumbi wa AICC unapofanyika mkutano huo wamesema moja ya vitu vinavyowavutia wajumbe wanaowatembelea ni bidhaa ya NMB Pesa Akaunti kutokana na hasa urahisi na wepesi wa kuifungua.

 NMB inatumia huduma hiyo, ambayo ni moja ya mikakati ya kufungua akaunti mpya za wateja ili kutekeleza ajenda yake ya kuwajumuisha Watanzania zaidi kifedha na kupeleka huduma zake vijijini.

 Aidha, maafisa wa NMB walisema wajumbe wanaotembelea banda lao wanavutiwa pia na gharama nafuu ya Sh1,000 ya  kuifungua akaunti ya NMB Pesa pamoja na uwezo wake wa kumwezesha anaye iimiliki kukopa hadi Sh500,000 kwa kutumia simu ya mkononi kupitia huduma ya Mshiko Fasta.

Kwa mujibu wa Meneja wa tawi la NMB Clock Tower Arusha, Praygod Mphuru, benki hiyo ni moja ya wadhamini wa mkutano huo wa siku tatu uliofunguliwa rasmi Jumatano na Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango.

Mkutano huo ulitanguliwa na kikao maalumu cha siku mbili ambacho nacho maafisa waandamizi wa NMB walishiriki kikamilifu kwa ajili ya kubalishana uzoefu, kujifunza vitu vipya na kwenda sambamba na mabadiliko yanayotokea katika tasnia ya usimamizi wa ndani duniani.

Mikutano hiyo miwili imeudhuriwa na takribani wajumbe 2000 wengi wakiwa Watanzania na wengine wakitoka katika nchi 26 za Afrika pamoja na mataifa kadhaa nje ya bara hili.

“Tunautumia pia mkutano huu kwa ukubwa wake kama fursa ya kuonyesha umahili wetu wa kutoa huduma bora, ubunifu mkubwa wa bidhaa na jinsi tunavyowekeza vilivyo katika teknolojia mpya za kisasa,” Mphuru alibainisha.

“Wote wanaotembelea banda letu wanakili kuvutiwa na utendaji wetu pamoja na ubora wa bidhaa zetu mbalimbali,”aliongeza na kusema hiyo ni pamoja na harakati za ujumuishaji kifedha kama ufunguaji wa akaunti mpya milioni 1.2 mwaka 2023.

NMB pia inatoa elimu kuhusu huduma yake ya benki bima (bancassurance) na bidhaa zake nyingi ambayo wajumbe  wa AFIIA 2024 wameisifia kwa uharaka wake wa kuchakata fidia za wateja, vifurushi lukuki shindani ilivyonavyo na wepese wa kuzilipia kinga zinazokatwa.

 Bidhaa nyingine kubwa kwenye banda la NMB ni ile ya nyumba ambayo kupitia kwake mteja anaweza kukopa hadi TZS bilioni moja na kutumia nyumba anayomiliki kupata mkopo.

“Wajumbe pia wamepata fursa ya kuyajua maeneo mengine ya huduma na bidhaa zetu mahsusi kwa kada mbalimbali za wateja ambazo ni pamoja na masuluhisho ya malipo, ufadhili wa biashara na mambo ya fedha za kigeni,” Mphuru alisema.

Vile vile wajumbe hao wa mkutano wa 20 wa AFIIA unaoratibiwa na Umoja wa Wakaguzi wa Ndani (IIA) Tanzania wamependezwa na NMB inavyozingatia suala la miamala isiyohusisha na fedha taslimu na mchango hilo katika kuendeleza uchumi wa kidijital nchini.

Bw Mphuru alisema uwekezaji mkubwa wa NMB katika kuboresha huduma na kuimarisha ufanisi kiutendaji umepelekea benki hiyo kuwa na miundombinu madhubuti ya kidijitali inayochangia kwa kiasi kikubwa ukinara wake sokoni.

Mafanikio hayo yote pamoja na kutokuwa na mshindani karibu katika kila kitu, alifafanua, ni matokeo ya uimara wa mizania unaotokana na msingi mzuri wa mtaji pamoja na ufadhili na ukwasi wa kutosha ilionao taasisi hiyo kubwa kuliko zote za fedha nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!