Wednesday , 22 May 2024
Home Kitengo Biashara Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar
BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the love

KAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi ya kilo 15 pamoja na majiko yake yenye sahani mbili kwa wahariri na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza leo 30 Aprili 2024 katika hafla fupi ya ugawaji wa mitungi hiyo  iliyofanyika Kigamboni Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Benoit Araman amesema lengo la kugawa mitungi kwa waandishi ni muendelezo wa kuunga mkono juhudi za za Rais Dk Samia Suluhu Hassan ambaye amedhamiria kuona matumizi ya nishati safi yanapewa kipaumbele.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Orxy Energies, Benoit Araman, akizungumza na wahariri na waandishi wa habari, kabla ya kukabidhi majiko na mitungi wa gesi ya kupikia, Kigamboni, Dar es Salaam, jana.

Ameeleza kuwa Oryx imekuwa na kampeni maalum ya kuhakikisha inaiwezesha jamii kutumia nishati safi,hivyo imekuwa ikigawa mitungi bure kwa makundi mbalimbali katika jamii na leo wamewafikia Wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari.

“Tunafahamu kuwa waandishi wa habari wanamchango mkubwa wa kuleta mabadiliko chanya, wanafanya kazi kubwa ya kuuhabarisha umma Hivyo kwa kutambua mchango wao hivyo Oryx tumeona ni busara pia kugawa mitungi kwa wadau hawa muhimu ambao wahariri na waandishi wa habari.

“Oryx Gas tukio hili tumelipa uzito mkubwa na hii inatokana na umuhimu wenu katika jamii yetu.Kwetu  vyombo vya habari vimekuwa daraja na kiunganishi kikubwa cha kufikisha taarifa zinazohusiana na nishati safi ya kupikia na hasa inayotokana na gesi ya oryx kwa jamii,” amesema Araman.

Amefafanua Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameeleza dhamira yake kubwani kuona ifikapo mwaka 2032 asilimia 80 ya Watanzania iwe inatumia nishati safi ya kupikia, Oryx Gas wamedhamiria kwa vitendo kufanikisha ndoto ya Rais.

“Tumekuwa tukigawa mitungi ya gesi na majiko yake bure kwa makundi mbalimbali yakiwemo ya baba na mama lishe, watumishi wa sekta ya afya na wajasiriamali.Tunayofuraha leo kukutana nanyi wahariri na waandishi wa habari katika tukio hilo la kuwakabidhi mtungi wa gesi wenye kilo 15 ukiwa na plate zake mbili

Aidha amesema kama ambavyo wamekuwa wakiahidi siku zote wataendelea na kampeni hiyo kadri ya uwezo wao lengo ni kuona wanafikiwa wananchi wengi zaidi

“Oryx Ges Tanzania mpaka sasa tumeshatoa mitungi ya gesi zaidi ya 33,000 maeneo mbalimbali nchini na kiasi cha Sh  bilioni 1.5 kimeshatumika,”amesema na kuongeza wanakabidhi mitungi hiyo kwa Wahariri na waandishi wakiamini  ni kundi lenye ushawishi mkubwa hivyo watahamasisha na kuwa mabalozi kwa jamii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hukumu mahakama kuu yabatilishwa kesi State Oil, Equity Bank Tz

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imebatilisha hukumu iliyotolewa...

BiasharaElimu

Benki ya Exim yazindua huduma ya ‘Exim Smart Shule’

Spread the love  KATIKA juhudi za kuboresha teknolojia za kidijitali katika sekta...

Habari Mchanganyiko

Geita, Mwanza waongoza kwa mbwa

Spread the loveNaibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema taarifa...

Biashara

Shinda mkwanja Meridianbet Kasino, ukicheza Expanse Tournament.

Spread the love  LION Kingdom ni sloti kutoka kasino ya mtandaoni yenye...

error: Content is protected !!