Wednesday , 22 May 2024
Home Kitengo Michezo Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa
Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love

 

LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu hii imefikia patamu kweli kweli kwani ni hatua ya nusu fainali, ambapo itafanikiwa kukutanisha klabu nne bora kabisa.

Usiku wa Ulaya utapigwa Jumanne ya leo na kesho Jumatano kama ilivyo kawaida ambapo leo utapigwa mchezo mmoja wa nusu fainali ya kwanza ya michuano hiyo kati ya Bayern Munich ambao watakuwa nyumbani kuwakaribisha Real Madrid, Kesho Jumatano ni Borussia Dortmund wakiwa nyumbani kuwaalika PSG.

Nusu fainali ya kwanza leo ambayo itawakutanisha miamba ya soka barani humo klabu ya Bayern Munich bingwa mara sita wa michuano hiyo akicheza na Real Madrid bingwa mara kumi na nne wa michuano hiyo, Unatarajiwa kua mchezo mkali kutokana na ubora wa vilabu hivo.

Mchezo kati ya Bayern Munich na Real Madrid ni mchezo wenye hadi kubwa sana barani ulaya mara nyingi wanapenda kuuita European Clasico kwa maana vinakutana vilabu ambavyo vina historia kubwa kwenye michuano hiyo mikubwa kabisa barani humo.

Vilabu hivo vimekutana mara 26 kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya ambapo klabu ya Bayern Munich imefanikiwa kushinda mara 12, Huku Real Madrid wakishinda mara 11 na mchezo huo ukimalizika kwa sare mara 3, Bayern Munich wakifunga mabao 41 Real Madrid wao wakifunga mabao 39.

Suka mkeka wako kwenye michezo mikali ya ligi ya mabingwa ulaya hatua ya nusu fainali itakayopigwa leo Jumanne na kesho Jumatano. Machaguo zaidi za 1000 yapo huku lakini vile vile Turbo Cash pia ipo. Unasubiri nini sasa? Ingia meridianbet na ubashiri sasa.`

Mchezo mwingine wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya  ambao utarindima ni kati ya klabu ya Borussia Dortmund dhidi ya klabu ya PSG kutoka kule nchini Ufaransa ni mchezo ambao pia unatazamiwa kua na uhsindani mkubwa, Kwani vilabu hivyo vyote vimeonesha ubora mkubwa mpaka kufikia hatua hii.

Borussia Dortmund wamefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali baada ya kuwapa kipigo cha kushangaza klabu ya Atletico Madrid, Kwani mchezo wa kwanza Atletico walipata matokeo ya ushindi wakiwa nyumbani mabao mawili kwa moja lakini Dortmund walipindua meza wakiwa katika dimba la nyumbani na kushinda kwa mabao manne kwa mawili.

PSG wao stori yao inafanana na ya wapinzani wao Dortmund kwani mchezo wa kwanza walipoteza nyumbani kwa mabao mawili kwa moja mbele ya Barca, Lakini walienda ugenini na kufanikiwa kupindua meza na kupata ushindi wa mabao manne kwa moja na kufanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali.

Vilabu hivi vimefanikiwa kukutana mara nne tu kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ulaya ambapo klabu ya Borussia Dortmund wakipata ushindi mara moja, Huku klabu ya PSG wao wakipata ushindi mara mbili na mchezo huo ukimalizika kwa sare mara moja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Unamalizaje ligi kama hujabeti na Meridianbet?

Spread the love JUMAPILI ya leo tutashuhudia mitanange kibao ambayo itamalizika kuanzia...

Michezo

Uingereza, Hispania, Italia na Ufaransa kinawaka leo

Spread the loveLIGI mbalimbali barani ulaya kuendelea leo na michezokadhaa mikali itakwenda...

Michezo

Leo mkwanja upo Meridianbet, usipishane nao

Spread the love  Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Michezo

Anza wikendi yako na Meridianbet, upige mkwanja wa maana

Spread the love Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

error: Content is protected !!