RAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri, kuwa Mkuu wa Majeshi (CDF)wa taifa hilo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya, Jenerali Kahariri ambaye kabla ya kupandishwa cheo alikuwa Luteni Jenerali, ameteuliwa kushika wadhifa huo leo tarehe 2 Mei 2024, akichukua mikoba ya Jenerali Francis Ogolla, aliyefariki dunia kwa ajali ya chopa (helkopta).
Jenerali Kahariri pia aliwahi kuwa Makamu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi. Baada ya Jenerali Ogolla kufariki dunia, aliteuliwa kukaimu kwa muda nafasi hiyo hadi alipoteuliwa rasmi na Rais Ruto.
“Rais Ruto leo amempandisha cheo Luteni Jenerali Charles Muriu Kahariri hadi cheo cha Jenerali na kumteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi.,” imesema taarifa ya Ikulu ya Kenya.
Katika hatua nyingine, Rais Ruto amemteua Meja Jenerali John Omenda, kuwa Makamu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, wakati Meja Jenerali Fatuma Gaiti akiteuliwa kuwa Kamanda wa Jeshi la Anga la Kenya.
Leave a comment