Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wizara ya Kilimo yapanga kutumia Sh. 1.2 trilioni 2024/25
Habari za Siasa

Wizara ya Kilimo yapanga kutumia Sh. 1.2 trilioni 2024/25

Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo
Spread the love

WIZARA ya Kilimo, imepanga kutumia bajeti ya Sh. 1.2 trilioni katika mwaka wa fedha wa 2024/25, huku ikitaja vipaumbele mbalimbali ili uandaaji wa mpango wa mageuzi ya kilimo wa miaka 25. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamebainika leo tarehe 2 Mei 2024, bungeni jijini Dodoma, wakati Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, anawasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa 2024/25, ambapo ameliomba Bunge kuidhinisha bajeti hiyo ya Sh. 1.2 trilioni.

Bashe ametaja vipaumbele vitakavyofanyiwa kazi kupitia bajeti hiyo, ikiwemo uendelezaji kilimo cha umwagiliaji kwa kukamilisha utekelezaji wa miradi 69 ya ujenzi na ukarabati wa mabwawa 14 na ujenzi wa skimu mpya 28 zenye hekta 69,505.

Waziri huyo wa Kilimo amesema katika mwaka ujao wa fedha, wizara yake imepanga kuimarisha upatikanaji wa mitaji kwa wakulima, kuongeza mauzo ya mazao ya kilimo ndani na nje ya nchi, kuimarisha uongezaji thamani na uhifadhi wa mazao kwa kushirikiana na sekta binafsi na ujenzi wa vituo vya masoko ya mazao.

Katika hatua nyingine, Bashe amesema sekta ya kilimo katika 2023 ilikua kwa asilimia 4.2 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 3.3 uliokuwa 2022. Pia, sekta hiyo imechangia asilimia 26.5 katika pato la taifa, wakati ikitoa ajira kwa wananchi kwa asilimia 65.6 na kuchangia asilimia 65 ya malighafi za viwanda.

Bashe amesema mauzo ya mazao ya kilimo nje ya nchi katika 2022/23 yamefikia dola za Marekani 2.3 bilioni ikilinganishwa na dola 1.2 bilioni katika 2019/20. Uzalishaji wa mazao katika msimu wa 2022/23 ulifikia tani 20,402,014.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RUWASA yachongewa, yateketeza mamilioni kwa maji yenye magadi

Spread the loveSAKATA la ukosefu wa maji wilayani Momba mkoani Songwe limezidi...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

error: Content is protected !!