Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni
Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa serikali za vijiji na mitaa mkoani humo, kutowauzia wananchi na wageni vitambulisho vya uraia (NIDA) kwani watakaobainika kuchukuliwa hatua kali. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe… (endelea).

Akizungumza jana  Jumatano na wananchi wa kijiji cha Itale kata ya Itale, Chongolo amesema kutokana na mkoa huo kupakana na nchi mbili Zambia na Malawi viongozi hao wanatakiwa kujiepusha na tamaa ya kuwauzia wananchi vitambulisho vilivyotolewa bure na serikali.

Chongolo amesema mkoa huo umepokea vitambilisho 365,000 ambavyo vitagawiwa bure kwa wananchi waliojiandikisha hivyo kiongozi atakayebainika kuwatoza wananchi kwa gharama yoyote atashughulikiwa.

Amewaonya viongozi hao kuacha tabia ya kuwapa vibali wananchi kutoka nchi jirani kwa lengo la kupata vitambulisho vya uraia kwani inahatarisha usalama wa nchi pamoja na kupunja keki ya watanzania ikiwepo upatikanaji wa mbolea ya ruzuku.

“Acheni kuwaruhusu wananchi wasio raia wa Tanzania kuwapa vibali vya uraia sambamba na kuwapa upenyo wahamiaji haramu kupata utambulisho hivyo tukikukamata utawajibika kwa mujibu wa sheria,” amesema Chongolo.

Amewataka watumishi wa Nida kwenda vijijini kuwasajili wananchi ambao hawana vitambulisho kwani zoezi hili bado ni endelevu nchini na kuacha kutoa barua za kuwaruhusu wananchi kutoka nchi jirani kujiandikisha kupata vitambulisho vya uraia.

“Wananchi wote waliosajiliwa na ambao hawajasajiliwa wanahaki ya kupata vitambulisho ili kuwarahisishia kupata huduma za jamii ambazo zinahitaji kuhudumiwa kwa kutumiwa vitambulisho hivyo,” amesema Chongolo

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Ileje, Faida Mgomi amesema watahakikisha wanawadhibiti na kuwachukia hatua viongozi watakaobainika wanauza vitambulisho hivyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!