Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Burudika Savage adondosha ‘your waist’ X King Perryy, Psycho YP
Burudika

Savage adondosha ‘your waist’ X King Perryy, Psycho YP

Spread the love

MSANII wa muziki wa Rap kutoka Nigeria, Savage a.k.a Savage tha Beast amerejea tena na wimbo wake mpya ‘Your Waist’ akiwa amegonga kolabo na King Perryy na PsychoYP. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Wimbo huo wa Hip-Hop na Rap una vionjo vya aina yake, huku mapigo ya Afro-Dancehall yaliyochagizwa na King Perryy ukizidisha utamu wa ngoma hiyo ambayo tayari imeshakuwa gumzo kwenye mitandao.

Video ya muziki ya wimbo huo inamuonesha Savage akiigiza kama mkurugenzi akiwa pamoja na Moustacheboy.

Wimbo wa kwanza wa Savage “Confident” akimshirikisha Buju uliunda utambulisho mzuri katika tasnia ya muziki, ikifuatiwa na albamu yake ya kwanza ya mwaka 2021 ‘Utopia’ iliyofungua njia yake na kuruhusu ushirikiano na mastaa mbalimbali wakiwemo Kojo Funds, Kida Kudz, Alpha P, Emtee na staa kutoka Kenya, Khaligraph Jones.

Savage ambaye ana umri wa miaka 27 sasa, ameanzisha timu ya wabunifu inayoitwa ‘Savage Space’ inayohusika katika mwelekeo wa ubunifu, mavazi – Savage Space Couture.

Awali, Savage alianza kufanya muziki akiwa na umri wa miaka 16 chini ya  bendi ya watu sita iliyoitwa “Team Nawty” iliyojumuisha marafiki kutokana na mapenzi yao kwa muziki.

Akiwa anatoka Uzere, Jimbo la Delta, Savage ni Mnigeria mwenye fahari anayewakilisha nchi yake ya asili na kuwatia moyo vijana wote kutoka Nigeria pamoja na Waafrika wenzake kupitia sanaa yake inayomnufaisha vilivyo.

1 Comment

  • A. UTANGULIZI

    1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Utekelezaji ya Mwaka 2022/23 na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mwenyendo wa Ujenzi wa Nyumba kwa Mwaka 2023/24. (Katika wana wa Simeoni, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, wale waliohesabiwa kama hesabu ya majina, kichwa kwa kichwa, kila mwanaume kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani – VITA IMEZIDI)

    2. Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kuniwezesha kuwasilisha Hotuba hii muhimu mbele ya Bunge lako Tukufu. Aidha, kwa namna ya kipekee kabisa namshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniamini kuendelea kusimamia Sekta ya Mwenyendo wa Ujenzi wa Nyumba ili kufikia matarajio ya Watanzania katika Sekta ya Ujenzi wa Nyumba Unaoisha na kuongeza mchango wake kwenye Pato la Taifa.

    3. Mheshimiwa Spika, vilevile kwa dhati nampongeza Mhe. Rais kwa namna anavyoiongoza Serikali ya Awamu ya Sita inayosimamia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025, ambapo mafanikio mengi yamepatikana katika sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Mwenyendo wa Ujenzi wa Nyumba ambapo WATANZANIA WOTE WANALALA KWENYE NYUMBA ZAO IFIKAPO USIKU WA SAA 1 BILA KUZINGATIA INAMILIKIWA YEYE MWENYEWE AU KUPANGA. Mafanikio hayo yameendelea kuitangaza nchi yetu siyo tu katika Bara la Afrika bali Duniani kote.

    4. Mheshimiwa Spika, ninaomba nitoe Rai kwa wananchi na Waheshimiwa Wabunge wote bila kujali itikadi za aina yoyote, tuendelee kuyaenzi mafanikio haya makubwa na kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.

    5. Mheshimiwa Spika, vilevile, nitumie fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru Viongozi Wakuu wa Kitaifa, ambao ni Makamu wa Rais, Dr. Philip Isdor Mpango pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dr Hussein Ali Mwinyi kwa hekima kubwa katika kumsaidia Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuongoza nchi yetu.

    6. Mheshimiwa Spika, pia, nimshukuru na kumpongeza Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.) kwani amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM na maelekezo mbalimbali ya Mhe. Rais pamoja na kusimamia vema shughuli za Sekta ya Mwenyendo wa Ujenzi wa Nyumba ndani na nje ya Bunge, AMBAO INAKUSUDI HADI KUFIKIA 2024 KILA MTANZANIA HATAKIWA KUJENGA TENA KWA MUJIBU WA SHERIA NA KUWAACHIA NHC NA TBA KUJENGA NYUMBA ZILIZO NA VIWANGO VYA KIMATAIFA.

    7. Mheshimiwa Spika, ninakushukuru wewe binafsi, Naibu Spika, Wenyeviti wa Bunge, Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge, akiwemo Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mwenyendo wa Ujenzi wa Nyumba na YAO Mhe. TAN L. VIAZI (Mb.) na Wajumbe wa Kamati hiyo. Kamati hii imefanya kazi nzuri na kutoa ushauri wa kuboresha mambo mbalimbali ikiwemo kupitia na kuchambua Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mwenyendo wa Ujenzi wa Nyumba na Taasisi zake kwa mwaka 2022/23.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BurudikaMichezo

Kizz Daniel aunguruma na EP mpya ‘Thankz alot’

Spread the loveMKALI wa muziki nchini Nigeria, Kizz Daniel ametoa EP yake...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Burudika

Piga makofi kwa Mr. Eazi …achomoka na ‘The Evil Genius’

Spread the loveMAKOFI kwa Mr Eazi! Staa wa Afropop, Mr Eazi ameachia...

Burudika

Kishindo cha Afro B katika “Wo wo wo” akiwa na Rich the Kid&Rimzee

Spread the loveSTAA ambaye alitambulishwa na ngoma maarufu, Afrowave ‘Drogba’, Afro B,...

error: Content is protected !!