Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Barrick yawataka wanawake kuchangamkia fulsa katika sekta ya madini
Habari Mchanganyiko

Barrick yawataka wanawake kuchangamkia fulsa katika sekta ya madini

Spread the love
MENEJA Mkuu wa Barrick Tanzania, Dk. Melkiory Ngido amewataka Wanawake kijiamini na kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya uchimbaji wa madini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Akiongea wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kwenye mgodi wa Barrick North Mara, Dk.Ngido  alisema Barrick  inayo programu maalumu ya kuwapa wanawake kipaumbele katika suala la ajira , kuwajengea uwezo wa shughuli za uchimbaji madini na kuwajengea mazingira bora zaidi ya  kazi.

“Msijisikie kuwa second class (daraja la pili), onesha kuwa mnaweza na naamini uwezo mnao,” alisema Ngido  katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na Wafanyakazi Wanawake kutoka mgodi huo.

Kwa upande wake,Meneja Mkuu wa mgodi huo, Apolinary Lyambiko, alisema anafurahishwa kuona idadi ya wafanyakazi wanawake katika mgodi huo imeongezeka uliganisha na miaka ya nyuma, na amewamiminia sifa kwamba wengi wao wanaonesha bidii na ufanisi mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yao kazini.

Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Dk. Melkiory Ngido

“Takwimu za mwaka jana na sasa zinaonesha kuna ongezeko la wafanyakazi wanawake katika mgodi wetu, na wengi wao wanafanya kazi nzuri. Hivyo tutaendelea kuwapa fursa, siyo tu kujishughulisha na uchimbaji, bali na kuwamotisha pia,” amesisitiza  Lyambiko na kuwataka kuendelea kuonesha uwezo mkubwa kazini na kujenga tabia ya kujiamini.

Lyambiko, alisema pia mgodi utaendelea kutekeleza sera yake ya kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa kuhakikisha vitendo hivyo vinakuwa  katika kiwango cha sifuri katika mgodi huo.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko
Katika kuadhimisha siku hiyo wafanyakazi wanawake wa mgodi huo walipata fursa ya kubadilishana mawazo na kujadili mada mbalimbali za maendeleo sambamba na  kupata burudani na kufurahi pamoja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!