Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Burudika Lojay aachia ‘moto’, kusafishia njia EP mpya ‘gangster romantic’
Burudika

Lojay aachia ‘moto’, kusafishia njia EP mpya ‘gangster romantic’

Spread the love

STAA wa Amapiano aliyetesa vilivyo na kibao chake ‘Monalisa’, Lojay sasa ameachia mtaani singo yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘MOTO’, ikiwa ni mwanzo wa kuelekea kutoa EP yake mpya GANGSTER ROMANTIC. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

‘MOTO’ ni wimbo wenye kisa cha kimapenzi, ambao unanogeshwa na uzuri wa ala za muziki zinazorindima kwa kasi na taratibu zikipishana na kuleta ladha ya aina yake.

Prodyuza wa wimbo huo ni Lojay mwenyewe, huku umaliziwaji ukifanywa na Elementz na AOD.

Mwongozaji wa video yake hiyo ni galacha, Des Gray kutoka Atlanta ambaye amepata kutia mikono katika kazi za mastaa wakubwa kama Quavo, Davido na Lil Baby.

Simulizi ya wimbo huo, ulioigizwa na Lojay mwenyewe, inaelezea kisa cha mapenzi, namna uhusiano ulivyoanza na kila aina ya nakshi kabla ya kuvunjika; imehaririwa kwa rangi ya samawati ili kuakisi uzito wa wimbo na kisa kilichopo ndani ya wimbo huo.

EP ijayo ya Lojay inawakilisha ulimwengu wenye misukosuko wa Lojay, unaoangaziwa na mambo ya shauku, tafakari ya kina, hofu kuu na mapenzi.

Ni tafakari ya kina juu ya mwaka uliopita wa maisha yake, huku Lojay akiwasilisha upya majarida yake ya dhati na maingizo ya hisia kuhusu mapenzi, maisha na huzuni katika shajara ya kusisimua, yenye tafakari, matarajio na fikira juu ya uhuru.

Wimbo wake wa ‘Canada’ alioutoa mwaka jana, akiwa amepiga kolabo na Kabza De Small na DJ Maphorisa, ulipata uungwaji mkono kutoka kwa Rolling Stone na DJ Target katika BBC Radio 1Xtra, huku ‘Leader’ alipongezwa na Jack Saunders wa BBC Radio 1.

Msanii huyo ataanza ziara nchini Australia mapema mwezi huu, ikiwa ni mwendelezo wa kung’arisha jina lake ulimwenguni akiwa ni staa anayetesa vilivyo kwenye mahadhi ya AfroBeats.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BurudikaMichezo

Kizz Daniel aunguruma na EP mpya ‘Thankz alot’

Spread the loveMKALI wa muziki nchini Nigeria, Kizz Daniel ametoa EP yake...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Burudika

Piga makofi kwa Mr. Eazi …achomoka na ‘The Evil Genius’

Spread the loveMAKOFI kwa Mr Eazi! Staa wa Afropop, Mr Eazi ameachia...

Burudika

Kishindo cha Afro B katika “Wo wo wo” akiwa na Rich the Kid&Rimzee

Spread the loveSTAA ambaye alitambulishwa na ngoma maarufu, Afrowave ‘Drogba’, Afro B,...

error: Content is protected !!