Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Burudika Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti
BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni katika uzinduzi wa taasisi ya Professa Jay Foundation pamoja na kuahidi kumgharamia matibabu ya upandikizaji wa figo Muasisi wa taasisi hiyo ambaye pia ni msanii wa Bongofleva, Joseph Haule ‘Profesa Jay’. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Mchango huo umetajwa leo tarehe 11 Desemba 2023 katika hafla ya uzinduzi wa Profesa Jay Foundation iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Akiwasilisha mchango wa Rais Samia, Naibu Waziri wa afya Dk. Godwin Mollel amesema mkuu huyo wa nchi amechangia 50 kwa ajili ya taasisi hiyo.

Pia amesema kama italazimika kwa msanii huyo kupandikizwa figo, atachangia gharama za matibabu hayo.

“Rais Samia ameahidi kuendelea kumsaidia Professa Jay na taasisi yake,’ amesema Dk. Mollel.
Amesema mbali na mchango huo wa Rais, yeye binafsi atachangia kiasi cha Sh milioni sita huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akichangia kiasi cha Sh 10 milioni.

Kwa upande wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mwenyekiti wake Freeman Mbowe ameahidi kuchangia Sh milioni tano, Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu amechangia Sh milioni mbili, Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika amechangia Sh milioni mbili huku Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Godbless Lema akiahidi kuchangia Sh milioni tatu.

Kwa upande wa wasanii akiwamo Ali Kiba na lebal yake ya Kings Music wameahidi kutoa kiasi cha Sh milioni tano na Kundi la Weusi wamechangia kiasi cha Sh milioni moja, Mwanadada Lady Jadee amnechangia Sh milioni mbili, Msanii wa filamu Gabo akishirikiana na Batuli, JB wamechangia Sh milioni mitani huku Chege na Temba (TNC) wakichangia Sh 1.7 Milioni

Kabla ya kuzinduliwa kwa taasisi hiyo inayolenga kuwasaidia watu wenye matatizo ya figo, tayari imeshakusanya ahadi za michango kiasi cha Sh 767 milioni kwa fedha, vifaa tiba na dawa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!