Tuesday , 18 June 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Wananchi waomba msaada ukamilishaji ujenzi wa sekondari
Elimu

Wananchi waomba msaada ukamilishaji ujenzi wa sekondari

Spread the love

WANANCHI wa Kijiji cha Muhoji, wilayani Musoma Mkoa wa Mara, wamewaangukia wadau wakiwaomba wawasadie michango ya hali na mali ili wakamilishe ujenzi wa Shule ya Sekondari Muhoji ili ianze kufanya kazi 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara…(endelea).

Ombi hilo limetolewa hivi karibuni na wananchi hao ambao wanaendelea na ujenzi wa sekondari hiyo kwa nguvu zao, ambapo kwa sasa wanakamilisha ujenzi wa vyumba viwili wa madarasa, ofisi moja ya walimu pamoja na vyoo.

Mbali na ombi hilo la wananchi, Ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, ambapo kijiji hicho kipo ndani yake, imeomba Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, itoe mchango wake kwa ajili ya kusaidia nguvu za wananchi.

“Ombi kutoka kijijini Muhoji, wazaliwa au watu wenye chimbuko la Kata ya Bugwema wanaombwa waungane na ndugu zao kukamilisha ujenzi wa Muhoji Sekondari. Wadau wengine wa maendeleo wanaombwa sana wachangie ujenzi wa shule hii,” imesema taarifa hiyo.

Katika hatua nyingine, Wakala wa Babarabara Mijini na Vijijini (TARURA) umeombwa isaidie ukamilishaji wa ujenzi wa barabara inayoingia Sekondari ya Muhoji, ikitokea barabara kuu la Murangi- Masinono-Manyamanyama (Bunda).

Muhoji Sekondari itakuwa ni Sekondari ya pili ya Kata ya Bugwema yenye vijiji vinne (Bugwema, Kinyang’erere, Masinono na Muhoji).

“Sekondari moja (Bugwema Sekondari) kwa Kata hii haitoshi, matatizo makuu yakiwa ni umbali mrefu wa kutembea kwa baadhi ya wanafunzi, na mirundikano madarasani,” imesema taarifa ya ofisi hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za SiasaTangulizi

Walimu 12,000 kuajiriwa mwaka huu, wa kike kupewa kipaumbele

Spread the loveKATIKA mwaka 2023/2024, Serikali inatarajia kuajiri walimu 12,000 wa masomo...

ElimuHabari za Siasa

Ukomo michango wanafunzi kidato cha tano 80,000

Spread the loveSERIKALI imesema ukomo wa michango kwa wanafunzi wanaojiunga kidato cha...

ElimuHabari Mchanganyiko

Dk. Biteko apongeza mikakati ya kuinua elimu Dodoma

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Dotto Biteko...

ElimuHabari za Siasa

Shigongo: Nafanya masters kwa kutumia kipaji pekee

Spread the loveMbunge wa Buchosa, Eric Shigongo (CCM) ameishukuru Serikali kwa kurejesha...

error: Content is protected !!