Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Biashara NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani
BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the love

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano wa kiutendaji na kampuni ya SILABU APP inayotoa huduma za masomo ya ziada kwa wanafunzi majumbani na kwa njia ya mtandao. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Makubaliano hayo yanalenga kushirikisha walimu wa taasisi hiyo kufikisha elimu ya fedha na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kwa wanafunzi wao.

Hatua hiyo inatajwa kuwa itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaongezea wanafunzi hao elimu na uelewa kuhusu masuala ya fedha na umuhimu wa kujiwekea akiba tangu wakiwa wadogo.

Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo ilifanyika leo Jumanne jijini Dar es Salaam ikihusisha mafunzo maalum kwa walimu wa taasisi hiyo yaliyotolewa na maafisa wa benki ya NBC.

Msimamizi wa Huduma za Elimu wa Benki ya NBC, Yoabu Ndanzi akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yametolewa kwa lengo la kuwajengea elimu ya kutosha walimu hao kuhusu huduma na program mbalimbali za benki hiyo mahususi kwa walimu na wanafunzi.

Pia yanatarajiwa kuwasaidia vema walimu hao kufikisha elimu hiyo kwa walengwa pindi wanapotimiza majukumu yao.

Akifafanua zaidi kuhusu mpango huo Msimamizi wa Huduma za Elimu wa Benki ya NBC, Yoabu Ndanzi alisema ushirikiano huu utatoa fursa kwa benki hiyo kuweza kuwafikia wanafunzi na walimu kwa urahisi zaidi, hatua ambayo itarahisisha suala zima la kuwajengea uelewa wanafunzi hao kuhusu elimu ya fedha sambamba na kutambua huduma za benki hiyo mahususi kwao.

Huduma hizo ni pamoja na akaunti ya Chanua na akaunti ya wanafunzi (Students Account) mahususi kwa watoto na wanafunzi huku pia walimu wakifikiwa kupitia Akaunti ya Mwalimu iliyobuniwa mahususi kwa ajili yao.

“Ushikiano huu unaboresha zaidi kifurushi cha pamoja kwa maana ya kwamba wakati SILABU wanapeleka darasa nyumbani, NBC pia tunatumia fursa hiyo kuingiza uzoefu wa benki nyumbani na hivyo kuwawezesha wanafunzi kunuafaika na elimu zote mbili ambazo zina umuhimu mkubwa sana kwa maisha yao,’’ alifafanua Ndanzi.

Mwanzilishi Mwenza wa kampuni ya SILABU APP inayotoa huduma za masomo ya ziada kwa wanafunzi majumbani na kwa njia ya mtandao, Adam Duma akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo.

Aliongeza kuwa kupitia mpango huo watoto watawekewa kiasi cha sh elfu 5 kila mwezi kwenye Akaunti zao za Chanua.

Alisema fedha hizo zinafadhiliwa na SILABU APP ili kuendeleza ushirikiano na wateja wao ambao ndio wanafunzi kila mwezi.

Akizungumzia ushirikiano huo Mwanzilishi Mwenza wa kampuni ya SILABU, Adam Duma alisema ushirikiano na NBC utahusisha walimu zaidi ya 1000.

Alisema pia utatoa fursa pia kwa walimu hao kunufaika na huduma mbalimbali za vipaumbele zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo akaunti ya Mwalimu huku pia kampuni hiyo ikinufaika kupitia matangazo ya huduma zake kupitia majukwaa mbalimbali ya taarifa za benki hiyo.

“Zaidi tunafarijika kuona kwamba sasa ‘package’ yetu ya mafunzo tunayoyatoa kwa wanafunzi wetu inakwenda kuongezewa kitu muhimu sana ambacho  ni elimu ya fedha.

“Kupitia elimu hii tunakwenda kuandaa kizazi kijacho ambacho kina uelewa wa kutosha kuhusu kujiwekea akiba, kutumia taasisi za fedha kujitengenezea mitaji sambamba na matumizi sahihi ya fedha zao,’’ alisema Duma.

Wakizungumza kwa niaba ya walimu wenzao walioshiriki mafunzo hayo, Mwalimu Sixtmund Byabato na Mwalimu Hellena Mabula pamoja na kuishukuru benki hiyo kwa kuwapatia elimu hiyo ambayo waliihitaji pia, walisema mafunzo hayo yamewaongezea uelewa wa kutosha utakaowawezesha kuwafundisha wanafunzi wao.

Mafunzo hayo pia yatawasaidia wao katika kufanikisha malengo yao hususani kupitia fursa mbalimbali zitolewazo na benki hiyo kupitia akaunti ya Mwalimu na akaunti ya Malengo huku pia wakitarajia kunufaika na mikopo rasmi ya taasisi hiyo.

Wakizungumzia mafunzo hayo walimu hao pamoja na kuishukuru benki hiyo kwa kuwapatia elimu hiyo ambayo waliihitaji pia, walisema mafunzo hayo yamewaongezea uelewa wa kutosha utakaowawezesha kuwafundisha wanafunzi wao.

Katika hatua nyingine, benki hiyo pia ilitumia fursa hiyo kuzindua msimu wa pili wa program yake ya kimichezo kwa watoto inayofahamika kama ‘Chanua Football Kliniki’ itakayofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, tarehe 1 Juni mwaka huu.

“Kupitia Chanua Football Kliniki watoto wote wenye akaunti ya Chanua watakuwa na sifa ya kushiriki program hii ya michezo. Vigezo kwa wenye akaunti mpya ni kuwa na ingizo la awali (initial deposit) la kiasi cha Shs 100,000 na kwa wale wenye akaunti hizi tayari kigezo ni kuwa na akiba isiyopungua kiasi cha Sh 200,000.’’

‘’Washiriki (Watoto na wazazi) watapata fursa ya kufurahia michezo na mafunzo mbalimbali, watapata jezi na Zawadi za jumla na za pekee, watashiriki chakula cha mchana pamoja na pia watashiriki michezo na wachezaji mashuhuri wa ligi kuu ya NBC,’’ alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Sloti ya Wild 81 malipo kwa njia 81 Meridianbet kasino

Spread the love Meridianbet kuna mchezo wa sloti wa kusisimua sanaambao utakufurahisha....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

error: Content is protected !!