SERIKALI inakusudia kufanya mapitio katika mitaala na programu za vyuo vikuu na vyuo vya ufundi stadi ili kuzifanyia maboresho kwa lengo la kuhakikisha wahitimu wake wanapata elimu bora itakayowawezesha nchi kupata rasilimali watu yenye ujuzi na maarifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Hayo yamebainishwa leo tarehe 7 Mei 2024, bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolph Mkenda, akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2024/25.
Prof. Mkenda amesema katika utekelezaji wa bajeti ya wizara yake ya 2024/25, watafanya mapitio ya mitaala 171, kuandaa mitaala mipya 18 pamoja na kuanzisha program za vipaumbele 145 za elimu ya juu. Pia, itaanzisha vituo vya elimu huruia ili kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu ya juu.
Katika hatua nyingine, Prof. Mkenda amesema wizara yake itahakiki mitaala 230 ya vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, ili kuhakikisha mafunzo yanayotolewa yanakidhi mipango ya nchi, soko la ajira la kitaifa na kimataifa na kuwawezesha wahitimu kujiajiri na kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira.
“Serikali itaendelea na mapitio ya Sheria ya Elimu ili iendane na Sera ya Elimu na Mfunzo 2014 toleo la 2023. Vilevile itafanya mapitio ya sheria na miundo ya taasisi mbalimbali ikiwemo COSTECH, TLSB, NECTA, VETA, TCU, NACTVET na TEA ili ziendane na maboresho ya sera na sheria na makubaliano mbalimbali ya kikanda na kimataifa,” amesema Prof. Mkenda.
Leave a comment