Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya
Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Spread the love

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameagiza huduma za dharura zipelekwe kwenye maeneo yaliyopata athari kutokana na kimbunga Hidaya kilichoikumb baadhi ya maeneo ya Pwani ya Tanzania. Anaripoti Mwanadishi Wetu, Dodoma … (endelea). Hayo yamesemwa leo tarehe 6 Mei, 2024 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye kikao cha dharura cha Kamati ya Maafa Kitaifa alichokiitisha kupokea taarifa ya hatua zilizochukuliwa kwenye maeneo yaliyopata athari.

“Rais ameelekeza hatua za haraka zichukuliwe katika maeneo yote yaliyoathiriwa na mvua zilizotokana na athari za kimbunga Hidaya ikiwa ni pamoja na kupeleka misaada,” amesema. Maeneo yatakayopelekewa misaada hiyo ni Mafia mkoani Pwani, Kilwa (Lindi) na Ifakara (Morogoro).

Waziri Mkuu ameliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lihakikishe linakamilisha zoezi la uokoaji katika maeneo ya Kilwa ambapo zaidi ya kaya 40 zimezingirwa na maji. “Jeshi la Zimamoto mmefanya kazi kubwa, hakikisheni maeneo yenye makazi yaliyozingirwa na maji, wakazi wake wanaondolewa na kupelekwa maeneo salama pamoja na kupewa huduma zote muhimu.”

Wakati huo huo, Waziri Mkuu ameziagiza Wizara za Ujenzi, Uchukuzi, Afya, Maji, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mambo ya Ndani ya Nchi, Ulinzi na Fedha zichukue hatua za dharura ili kuhakikisha hakuna madhara zaidi yanatokea katika maeneo yaliyopatwa na athari.

“Wizara ya Ujenzi endeleeni kuchukua hatua zote za dharura zinazohitajika kuhakikisha maeneo ya barabara yaliyokatika yanarekebishwa na huduma za usafiri zinarudi haraka.”

Waziri Mkuu amepongeza jitihada zinazofanywa na Idara ya Menejimenti ya Maafa kwa kuendelea kufanya uratibu katika maeneo yote yaliyoathirika na kuwataka waendelee na uratibu katika maeneo yaliyopata madhara kuanzia juzi.

“Ongezeni nguvu katika maeneo ya Ifakara, Kilwa na Mafia na kuhakikisha wananchi wote walioathiriwa wanakuwa katika maeneo salama na wanapata huduma zote za msingi za kijamii.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameiagiza Kamati ya Maafa ya Kitaifa izisimamie Kamati za mikoa na Wilaya ili misaada inayotolewa kwa waathirika iwafikie walengwa. “Kamati ya Kitaifa izielekeze Kamati za Mikoa na Wilaya zisimamie misaada yote ya waathirika ili ifike kwa wahusika, baadaye hali ikisharejea, tutataka tupate taarifa ya kina na jinsi ilivyotumika,” amesisitiza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!