Wednesday , 6 December 2023
Home Kitengo Maisha Burudika Piga makofi kwa Mr. Eazi …achomoka na ‘The Evil Genius’
Burudika

Piga makofi kwa Mr. Eazi …achomoka na ‘The Evil Genius’

Spread the love

MAKOFI kwa Mr Eazi! Staa wa Afropop, Mr Eazi ameachia albamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la ‘The Evil Genius’ iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Video za albamu hiyo imechukuliwa katika maeneo na nchi tofauti kama,  Ouidah na Cotonou, Benin;  Kigali, Rwanda;  Accra na Kokrobite, Ghana;  Lagos, Nigeria;  London;  Los Angeles;  na New York City.

Albamu hiyo  ‘The Evil Genius’ huangazia baadhi ya kazi za kibinafsi za Mr Eazi, anapozama kwa kina katika mada kama vile mapenzi, usaliti, upweke, na familia, zinazoonyeshwa kupitia vitendo vitatu tofauti.

Washiriki katika kazi hiyo na nchi wanazotoka kwenye mabano ni Angelique Kidjo (Benin), Tekno (Nigeria), Efya (Ghana), Whoisakin (Nigeria), Joeboy (Nigeria), na washindi mara tatu wa Grammy Soweto Gospel Choir (Afrika Kusini).

Kwa upande wa watayarishaji, walikuwa pamoja na Kel-P (Nigeria), Knucks (U.K.), Michael Brun (Haiti), Andre Vibez (Nigeria), Yung Willis (Nigeria), Nonso Amadi (Nigeria/Canada), KillBeatz (Ghana), M.O.G Beatz (Ghana), E Kelly (Nigeria), Type A (Nigeria), Stikmatik (U.K.), Phantom (Nigeria), Beat Butcha (U.K.), Venna (U.K.), KDream (Nigeria) na Mr Eazi mwenyewe.

Katika kuonyesha Mr Eazi ni mwamba wa kuchanganya ladha, ndani yake yupo staa kutoka Afrika Mashariki – Kenya – Alphonce Odhiambo ‘Alpha ODH’ ambaye amemshirikisha kwenye kibao ‘Advice’.

Kwa upande wa usanifu wa jalada la albamu hiyo, Mr Eazi alishirikiana na mwanamitindo maarufu wa Nigeria, mbunifu na mpiga picha Daniel Obasi, anayejulikana kwa kazi yake nzuri alizowafanyia mastaa Beyoncé na Louis Vuitton.

https://empawaafrica.lnk.to/TheEvilGenius

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Burudika

Kishindo cha Afro B katika “Wo wo wo” akiwa na Rich the Kid&Rimzee

Spread the loveSTAA ambaye alitambulishwa na ngoma maarufu, Afrowave ‘Drogba’, Afro B,...

Burudika

Mr. Eazi aachia Advice ikiwa ni ujio wa albam mpya

Spread the loveSTAA wa muziki kutoka nchini Nigeria, Mr.Eazi ni gwiji linapokuja suala...

Burudika

Stonebwoy adondosha ‘Dimension’ kolabo na Stormzy, Davido…

Spread the loveMSANII mahiri wa Afro- Dancehall kutoka nchini Ghana aliyesainiwa na...

Burudika

Mr Eazi, DJ Edu kuachia ngoma mpya ya Wena

Spread the loveBAADA ya kutangaza habari kubwa za ujio wa project ya...

error: Content is protected !!