Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Burudika Mr. Eazi aachia Advice ikiwa ni ujio wa albam mpya
Burudika

Mr. Eazi aachia Advice ikiwa ni ujio wa albam mpya

Spread the love

STAA wa muziki kutoka nchini Nigeria, Mr.Eazi ni gwiji linapokuja suala la kuachia rekodi tamu yenye burudani ya kipekee kwa jamii na sasa ameachia kitu kipya. Anaripoti Joseph Shaluwa…(endelea).


“Advice,” ni kazi mpya kutoka staa huyo ambayo imetiwa mkono na lebo maarufu nchini Ghana, M.O.G. Beatz, ikiwa inapatikana katika albamu inayokwenda kwa jina la ‘The Evil Genius’, itakayotoka rasmi Oktoba 27, mwaka huu.

Advice unawataja baadhi ya watu mashuhuri ulimwenguni wakiwemo Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila na Ken Saro-Wiwa, mwandishi na mwanaharakati wa Nigeria ambaye mwaka 1995 alichomoza zaidi ndani na nje ya nchi ya Nigeria.

“Nilikuwa nikitoka mahali pa kuwa na nguvu hiyo,” Mr. Eazi anasema.

Katika albamu hiyo ambayo ina ngoma 16, staa wa muziki nchini Kenya,  Alphonce Odhiambo maarufu kama Alpha ODH, ameshirikishwa.

Mr. Eazi alichagua mwenyewe wasanii 13, wanaowakilisha nchi nane za Afrika, akiwaalika kushirikiana katika mchakato anaoutaja kuwa ‘usio rasmi na wa silika’.

“Kualika wasanii kwa ajili ya albamu hii kulitokana na shauku yangu ya ubunifu na kujitanua zaidi katika nchi zetu za Kiafrika.  Kazi za sanaa hufungua mawazo, hisia, na nishati ndani ya muziki wangu,” anasema Eazi.

Kazi za sanaa iliyoundwa kwa ajili ya albamu hiyo zitaonyeshwa katika maonyesho ya hisia nyingi, ambayo yataanza kutumika Accra, Ghana.

Ni albamu iliyorekodiwa katika kipindi cha miaka miwili katika maeneo mbalimbali kama Ouidah na Cotonou, Benin; Kigali, Rwanda; Accra na Kokrobite, Ghana; Lagos, Nigeria; London; Los Angeles; na New York City, Marekani.

https://youtu.be/OFpHSoaeSr8?si=XuaPk569UxdWs8fQ

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BurudikaMichezo

Kizz Daniel aunguruma na EP mpya ‘Thankz alot’

Spread the loveMKALI wa muziki nchini Nigeria, Kizz Daniel ametoa EP yake...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Burudika

Piga makofi kwa Mr. Eazi …achomoka na ‘The Evil Genius’

Spread the loveMAKOFI kwa Mr Eazi! Staa wa Afropop, Mr Eazi ameachia...

Burudika

Kishindo cha Afro B katika “Wo wo wo” akiwa na Rich the Kid&Rimzee

Spread the loveSTAA ambaye alitambulishwa na ngoma maarufu, Afrowave ‘Drogba’, Afro B,...

error: Content is protected !!