Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wananchi watakiwa kuondoka mabondeni kujiepusha na mvua za El Nino
Habari MchanganyikoTangulizi

Wananchi watakiwa kuondoka mabondeni kujiepusha na mvua za El Nino

Spread the love

 

SERIKALI imewatahadharisha wananchi kuacha kujenga na kufanya shughuli za kijamii kwenye maeneo ya bondeni ili kuepukana na athari za mafuruko zinazoweza kutokea na kuwasababishia madhara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Tahadhari hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis wakati akijibu maswali bungeni jijini Dodoma, leo Septemba 05, 2023.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Stella Ikupa aliyetaka kujua Serikali imejipangaje kukabiliana na athari za mvua za El – Nino zinazotarajiwa kunyesha kuanzia Oktoba mwaka huu, Khamis alisema elimu itaendelea kutolewa kwa wananchi ili waache kufanya maeneo ya mabondeni kuwa makazi.

“Ni kweli panapokuwa na mvua kubwa kama hizi mara nyingi hutokea madhara ambayo yanaharibu makazi na kugharimu maisha ya watu, hivyo Serikali katika kipindi hiki tunawapa elimu wasijenge kwenye maeneo ambayo yanakaa maji na kama wana mpango huo basi waondoke ili mvua zitakaponyesha wasipate madhara,” alisisitiza.

Awali akijibu swali la msingi la Mbunge wa Nungwi, Simai Hassan Sadiki aliyetaka kujua mkakati wa dharura wa kunusuru athari za mabadiliko ya tabianchi eneo la Nungwi, Zanzibar, Naibu Waziri Khamis aliwahimiza wananchi kuendelea kupanda mikoko katika fukwe za bahari ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis

Alifafanua kuwa Serikali inaendelea kuhamasisha wananchi visiwani humo kufanya shughuli endelevu zisiharibu mazingira zikiwemo ulimaji na uvunaji wa mwani usioharibu fukwe.

Alisema kwa kutambua changamoto za athari za mabadiliko ya tabianchi, tayari Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeanza kuchukua hatua za kukabiliana nazo.

“Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 SMZ imetenga kiasi cha shilingi milioni mia sita na hamsini kwa ajili ya kufanya tathmini ya awali ya kuzuia changamoto za athari za mabadiliko ya tabianchi,” alisema.

Aidha, Naibu Waziri Khamis amesisitiza kuwa Serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na SMZ zitashirikiana katika kutafuta fedha zaidi ili kudhibiti uharibifu unaotokea eneo la Nungwi.

Hivi karibuni Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitangaza kuanza kwa mvua za El – Nino Oktoba hadi Desemba 2023 na kutahadharisha kuweza kusababisha madhara kwa binadamu na mazingira ikiwemo mafuriko.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

error: Content is protected !!