Tuesday , 5 December 2023
Home Kitengo Maisha Burudika Kishindo cha Afro B katika “Wo wo wo” akiwa na Rich the Kid&Rimzee
Burudika

Kishindo cha Afro B katika “Wo wo wo” akiwa na Rich the Kid&Rimzee

Spread the love

STAA ambaye alitambulishwa na ngoma maarufu, Afrowave ‘Drogba’, Afro B, ameachia video yake mpya ya kibao “Wo Wo Wo (Ebony)” – ikiwa ni kolabo na Mmarekani, Rich The Kid, na msanii wa muziki wa rap nchini Uingereza, Rimzee.  Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ni kolabo ya kimataifa kwani inajumuisha mastaa kutoka mabara tofauti ulimwenguni.

Afro B ni raia wa Ivory Coast ambaye kwa Sasa makazi yake yapo nchini Uingereza katika Jiji la London.


Kabla ya kibao hiki, msanii huyo amepata kufanya kazi na mastaa wengine wa muziki wakiwemo, Wizkid, Slim Jxmmi (Rae Sremmurd), DJ Snake, Sukihana na wengineo.

Tangu wakati huo, amepata kuungwa mkono na Billboard, BET, BBC Radio 1, Capital, Hot 97, Power 105 na The Fader, Rolling Stone & NME ++.

“Wo Wo Wo (Ebony)” ni ufunguzi wa safari mpya ya kuhanikiza hadhira yake, mwakani 2024.

“Mambo makubwa yanakuja. Huu ni mwanzo tu. Mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwakweli,” anasema Afro B akizungumzia kazi yake hiyo mpya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Burudika

Piga makofi kwa Mr. Eazi …achomoka na ‘The Evil Genius’

Spread the loveMAKOFI kwa Mr Eazi! Staa wa Afropop, Mr Eazi ameachia...

Burudika

Mr. Eazi aachia Advice ikiwa ni ujio wa albam mpya

Spread the loveSTAA wa muziki kutoka nchini Nigeria, Mr.Eazi ni gwiji linapokuja suala...

Burudika

Stonebwoy adondosha ‘Dimension’ kolabo na Stormzy, Davido…

Spread the loveMSANII mahiri wa Afro- Dancehall kutoka nchini Ghana aliyesainiwa na...

Burudika

Mr Eazi, DJ Edu kuachia ngoma mpya ya Wena

Spread the loveBAADA ya kutangaza habari kubwa za ujio wa project ya...

error: Content is protected !!