Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Maisha Burudika Kizz Daniel aunguruma na EP mpya ‘Thankz alot’
BurudikaMichezo

Kizz Daniel aunguruma na EP mpya ‘Thankz alot’

Spread the love

MKALI wa muziki nchini Nigeria, Kizz Daniel ametoa EP yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Thankz Alot’, ambayo inakwenda kuthibitisha ubora wake katika muziki. Anaripoti Joseph Shaluwa… (endelea).

Katika EP hiyo yenye ujazo mkubwa wa ubora, inajumuisha nyimbo nne kali, maalum kwa mashabiki wake ulimwenguni mwote, ambao wamekuwa naye kwa kipindi cha takribani muongo mmoja tangu aanze muziki.

Tangu ilipoachiwa hewani EP hiyo, imeonesha kupokelewa kwa upendo mkubwa na mwitikio chanya kwa wingi katika nchi za Afrika Mashariki na kwingineko duniani.

Akitoa shukrani zake kwa mapokezi mazuri ya kazi yake hiyo, Kizz Daniel anasema: “Ninashukuru sana kwa upendo na uungwaji mkono ambao nimepata kutoka kwa mashabiki wangu katika kipindi chote kwenye karia hii ya muziki. ‘Thankz Alot’ ni njia mojawapo ya kurudisha  shukrani zangu kwa mashabiki wangu. Asanteni sana.”

EP ya ‘Thankz Alot’ ina nyimbo nne za kusisimua, kila moja ikionyesha umwamba wa Kizz Daniel na mtindo wa kipekee wa muziki.

Nyimbo hizo ni pamoja na “Sooner”, “Showa”, “Too Busy to Be Bae” na “Twe Twe” ambayo Remix yake amefanya kolabo la galacha wa muziki nchini Nigeria, Davido. EP hiyo tayari inapatikana katika  digital platforms zote.

 https://youtu.be/041PlAGNMsQ?si=JHNie1FBKgl1h7Gz

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Uingereza, Hispania, Italia na Ufaransa kinawaka leo

Spread the loveLIGI mbalimbali barani ulaya kuendelea leo na michezokadhaa mikali itakwenda...

Michezo

Leo mkwanja upo Meridianbet, usipishane nao

Spread the love  Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Michezo

Anza wikendi yako na Meridianbet, upige mkwanja wa maana

Spread the love Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Habari MchanganyikoMichezo

Arafat atoka bima na kurejea kwenye benki

Spread the loveRais wa Zanzibar Hussein Mwinyi amemteua Arafat Ally Haji kuwa...

error: Content is protected !!