Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Tangulizi Rais Samia kufanya ziara Ufaransa, Ubelgiji
Tangulizi

Rais Samia kufanya ziara Ufaransa, Ubelgiji

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajia kuondoka nchini kuelekea Ufaransa na baadaye Ubelgiji kwa ajili ya ziara ya kikazi katika nchi hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 9 Februari, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imesema, Rais Samia akiwa nchini Ufaransa anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaojadili kuhusu Rasilimali Bahari Duniani.

Pia Rais Samia atashuhudia utiaji saini baina ya Serikali ya Tanzania na Ufaransa katika sekta za miradi ya maendeleo, ushirikiano katika masuala ya uchumi wa buluu, usalama wa bahari, sekta ya usafiri na maendeleo endelevu.

Aidha, pamoja na masuala mengine, Rais Samia anatarajiwa kuzungumza na Watanzania waishio nchini Ufaransa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

Habari za SiasaTangulizi

Kinana: Hatukubali kushutumiwa kwa uongo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema viongozi wa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

error: Content is protected !!