Saturday , 18 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia
Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the love

WAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya mikoa ya ukanda wa Pwani ikiwamo Lindi, Mtwara, Pwani na Dar es Salaam, tayari baadhi ya wakazi wa kisiwa cha Mafia mkoani Pwani wamepoteza makazi yao kutokana na athari ya kimbuga Hidaya kilichotokea jana Ijumaa usiku. Anaripoti Faki Sosi… (endelea).

Kimbunga hicho kilichokadiriwa kulichoambatana na mvua kubwa, kimeezua paa za nyumba za wakazi wa kisiwa hicho, huku nyumba nyingine zikivunjika kwa kudondokewa na miti ya minazi na miembe.

 

Taarifa za awali kutoka kwa wakazi hao, zinasema kimbunga hicho kimeleta athari kubwa kwa wakazi wa Kata za Jibondo, Kiegeani na Kilindoni.

Akizungumzia hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Sauda Mangosongo ameieleza MwanaHALISI Online kuwa tayari timu yake ya usalama ipo kwenye sehemu yalipotokea maafa hayo hivyo baadaye atatoa taarifa juu juu ya tukio hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua bima ya afya kwa wakulima

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na kampuni...

Habari Mchanganyiko

Makamba awasili China kwa ziara ya kikazi

Spread the loveWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Ethiopia yafungua njia ujenzi wa ubalozi Dodoma

Spread the loveSerikali ya Tanzania imeipongeza Serikali ya Ethiopia kwa kuweka historia...

error: Content is protected !!