Saturday , 18 May 2024
Home Kitengo Biashara Exim Bank yaendeleza malipo ya kidijitali na Chef’s Pride Dodoma
Biashara

Exim Bank yaendeleza malipo ya kidijitali na Chef’s Pride Dodoma

Spread the love

 

BENKI ya Exim imeingia makubaliano na Mgahawa wa Chef’s Pride ikiwa ni pamoja na kutoa punguzo na ofa mbalimbali kwa wateja wake watakaotumia kadi za benki hiyo kufanya miamala ya malipo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Tukio hili pia liliambatana na uzinduzi rasmi wa mgahawa wa Chef’s Pride uliofanyika jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule aliyeipongeza benki ya Exim ushirikiano hayo.

“Serikali tunawapongeza benki ya Exim kwa maamuzi yao ya kuja kuwekeza Dodoma kama sehemu ya kusogeza huduma kwa wateja wao popote pale walipo. Tunahimiza na kuwakaribisha wawekezaji wengine kuiga mfano huu wa Exim Bank,” alisema Rosemary.

Akizungumzia mashirikiano hayo, Meneja Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim, Kauthar D’souza alisema, “Benki ya Exim tumekuwa na kawaida ya kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora za kifedha kwendana na mabadiliko ya kidijitali yanayotokana na maendeleo ya teknolojia. Tunafuraha kubwa kuungana leo na mgahawa wa Chef’s Pride katika kuboresha huduma zetu kwa wateja hasa matumizi ya kadi za benki yetu.”

Mkuu wa Idara ya Huduma za Kadi na Malipo wa Exim Bank, Paritosh Babla (kulia), na Mkurugenzi Mtendaji wa Mgahawa wa Chef’s Pride, Salim Mahsen Al Amry, wakisaini makubaliano ya ushirikiano katika uzinduzi rasmi wa tawi la Chef’s Pride Dodoma.

Ushirikiano huu pia unalenga kukuza urahisi na usalama wa miamala ya wateja wa benki hiyo ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za benki ya Exim kuongeza matumizi ya kufanya miamala kupitia kadi zao ili kuwapa  fursa wateja wake kufurahia ofa mbalimbali pamoja na punguzo. Pia, kwa yule ambaye hana akaunti na Exim Bank anaweza kutembelea tawi lolote la Exim na kupata kadi yake ya malipo ya kabla (Prepaid) ili kuweza kufurahia ofa hii.

Kupitia huduma hii, mteja ataweza kutumia kadi yake kufanya miamala ya malipo na kupata punguzo maalumu na ofa zingine utakapofanya miamala ya malipo kwa kutumia kadi yetu.

Akielezea baadhi ya ofa hizo, Kauthar alisema, “Wateja watakaowahi kupata kadi za Exim na wale watakaotumia fedha zaidi wataondoka na zawadi za vocha na kadi za malipo ya kabla yenye fedha ndani yake.”

Exim Bank imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini katika sekta kadhaa kama vile uchumi, uwezeshaji, elimu, afya, mazingira, usalama, na teknologia kupitia sekta binafsi pamoja na serikali ya Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB ‘yafunga ndoa’ na wanawake wanaomiliki shule, vyuo Tanzania

Spread the loveBENKI ya NMB imeingia makubaliano rasmi (MoU) na Chama cha...

Biashara

Cheza kasino sloti ya Fruit O Rama malipo unayapata kwa njia 10

Spread the love Karibu kwenye burudani ya kasino ya mtandaoni isiyozuilikayenye kutawaliwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua bima ya afya kwa wakulima

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na kampuni...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Total Energies yawekeza bilioni 17 kusambaza gesi ya kupikia

Spread the loveILI kurahisisha upatikanaji wa gesi ya kupikia kwa gharama nafuu...

error: Content is protected !!