Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia
Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Joseph Selasilini, alimpe fidia ya fedha kiasi cha Sh. 80 milioni, aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia, kwa kosa la kumchafua. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Amri hiyo ilitolewa juzi tarehe 2 Mei 2024 na mahakama hiyo mbele ya Hakimu mkazi Aron Lyamuya, katika hukumu ya kesi ya madai namba 87/2023 iliyofunguliwa na Mbatia dhidi ya Sesalini, akimtaka alimpe fidia kwa kumchafua kwa kutoa tuhuma mbalimbali dhidi yake.

Amri hiyo kwa Selasini kumlipa fidia Mbatia pamoja na kumuomba radhi katika ukurasa wa mbele wa gazeti linalosambazwa nchi nzima au kwenye eneo alikotoa tuhuma dhidi yake wilayani Musoma mkoani Mara, imetolewa baada ya Selasini kushindwa kuthibitisha mahakamani tuhuma alizotoa.

Pia mahakama hiyo imemuamuru Selasini kulipa gharama za uendeshaji kesi hiyo ya madai.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Ijumaa, Wakili wa Mbatia, Hudson Mchau alisema wamewasilisha mahakamani maombi ya utekelezaji wa hukumu hiyo.

Naye Mbatia alisema hukumu hiyo inadhihirisha kwamba jaribio la kutweza utu wake limekwama.

“Marafiki zangu wote wakiwa ni watoto wa mama Tanzania wanaoamini katika kukuza na kuheshimu utu wa binadamu, jaribio la kutweza utu wangu limeshindwa mahakama imeongea, asante sana mahakama,” alisema Mbatia.

Mvutano kati ya Mbatia na Selasini uliibuka baada ya mwanasiasa huyo aliyekuwa mwenyekiti wa NCCR-Mbatia kung’olewa madarakani huku Selasini akituhumiwa kusuka mpango huo ingawa mara kadhaa amekuwa akikanusha akisema ameondolewa kupitia vikao vya chama hicho.

Selasini katika nyakati tofauti amekuwa akimtuhumu Mbatia kwa matumizi mabaya ya madaraka akiwa mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, ikiwemo kwa kuuza nyumba za chama na kuwaomba rushwa wanawake wanaotaka nafasi ya ubunge viti maalum kupitia chama hicho.

Hata hivyo, Selasini ameshindwa kuthibitisha mahakamani tuhuma hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!