Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa
Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the love

ALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa Mkulo amefariki dunia leo tarehe 4 Mei 2024 katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Anaripoti  Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mke wa marehemu, Julie Mkulo msiba upo nyumbani kwa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, taarifa hiyo imeeleza shughuli zote za mazishi zitakuwa katika Msikiti wa Maamur leo Jumamosi.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa maziko yatakuwa kesho Jumapili tarehe 5 Mei 2024 Kilosa mkoani Morogoro.

Mkulo ambaye alikuwa ni mbunge mstaafu, aliongoza kwa miaka 10 jimbo la Kilosa na katika kipindi hicho alishika nafasi ya waziri wa fedha kuanzia mwaka 2007 hadi 2012 alipotemwa na Rais Jakaya Kikwete.

Mkulo alitangaza kutogomea tena katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na nafasi yake ikachukuliwa na Mbunge Mbaraka Bawaziri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!