WIZARA ya Maji nchini Tanzania, imeanza mikakati ya kihakikisha inamaliza tatizo la maji mijini na vijijini kwa kuingia mkataba wa kusambaza vifaa vya maji na Kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Mkataba huo umesainiwa leo Jumatano, tarehe 9 Februari 2022, jijini Dodoma baina ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mhandisi Anthon Sanga na mkurugenzi wa kampuni hiyo, Imran Karmali.
Mhandisi Sanga amewataka walioshinda zabunu hizo za kusambaza vifaa hivyo kuhakikisha wanakamilisha na kukabidhi kwa wakati na isizidi mwezi wa tano ili kuendana na kasi ya Rais Samia Suluhu Hassani ya kuhakikisha miradi inamalizika kwa wakati.
Naye Karmali amesema wao wamelipokea agizo hilo la kukamilisha na kukabidhi vifaa hivyo kwa wakati.
Aidha ameishukuru Serikali kwa kuaminiwa na kwamba wao kama Kampuni hawataingusha katika hilo na ikiwezekana kabla ya mwezi wa tano kila kitu kitakuwa tayari, Ikizingatiwa GF inayomiliki kiwanda cha kutengeneza Magari hapa hapa nchini Tanzani kilichopo Kibaha mkoani Pwani wamejipanga vizuri.
Amesema, kupitia miradi ya maji wao itakuwa kazi nyepesi kwao kwani kupata kwa zabuni hiyo kutaongeza tija katika kiwanda chao na kwa kuwa wana wataalamu wa Kitanzania itakuwa rahisi kukamilisha mahitaji kwa wakati.
Leave a comment