October 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Miradi Dodoma: Mbunge Ditopile amfagilia Rais Samia

Spread the love

 

MBUNGE wa Viti Maalum (CCM), Mariam Ditopile amesema Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya muda mfupi tangu aingie madarakani anazidi kuwaumbua wale wote waliombeza kuhusu uendelezaji wa miradi ya kimkakati Jiji la Dodoma iliyo asisiwa na mtangulizi wake Hayati John Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Ditopile ameyasema hayo leo Jumatano tarehe 9 Februari 2022, baada ya Hafla ya Rais Samia kuweka Jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje katika mji wa Dodoma.

Barabara hiyo itatoka Ihumwa-Matumbulu-Nala-Veyula-Ihumwa Kilometa 112.3.

“Nampongeza kidhati Rais Samia kwa kuendelea kutimiza ahadi zake kwa vitendo za kuendeleza miradi yote ya kimkakati iliyoasisiwa na Hayati John Magufuli Jijini Dodoma, wote ni mashahidi miradi inaendelezwa kwa kasi kubwa sana”

“Yalikuwepo maneno kwamba Hayati ameondoka na miradi itasimama au haitafanyika lakini sasa ni tofauti, miradi yote inaendelezwa. Mradi huu wa ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje wa Jiji la Dodoma ni mradi ulisubiriwa kwa Hamu na wana Dodoma utalibadilisha hili jiji letu”

“Miradi mwingine unaendelezwa na Rais Samia Jijini Dodoma ni ujenzi wa Hospitali Mpya ya Jiji la Dodoma na tayari Rais Samia ametoa zaidi ya Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wake kuanza, sisi wana Dodoma tunamshukuru na kumpongeza Sana,” amesema

Mbunge huyo amesema Rais Samia anaonyesha kwa vitendo anayo nia ya dhati ya kuendeleza miradi yote ya mtangulizi wake, nawasihi watanzania tupuuze maneno ya watu wachache wasioitakia mema Nchi yetu, Rais Samia atatekeleza miradi yote aliachiwa tena kwa kasi kubwa na ufanisi”

Rais Samia aliingia madarakani tarehe 19 Machi 2021, baada ya Rais Magufuli kufariki dunia siku mbili nyuma na mwili wake kuzikwa kwao, Chato mkoani Geita 26 Machi 2021.

error: Content is protected !!