December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ampa siku 90 DED Karatu

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amempa miezi mitatu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu mkoani Arusha (DED), Karia Rajabu, kuhakikisha ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo uwe umekamilika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha…(endelea).

Rais Samia ametoa agizo hilo leo Jumapili, tarehe 17 Oktoba 2021, akizungumza na wananchi wa Jiji la Arusha, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Kiongozi huyo wa Tanzania, ametoa agizo hilo baada ya ujenzi wa hospitali hiyo ulioanza 2019 kukwama, licha ya Serikali kutoa fedha zote.

“Karatu kuna hospitali ya wilaya ambayo imeanza kujengwa tangu 2019, fedha zote zimetolewa hospitali haijaisha, mkurugenzi wa Karatu nakupa meizi mitatu sababu fedha yote unayo sioni kwa nini hospitali haijaisha,” amesema Rais Samia na kuongeza:

“Mwaka wa pili sasa kinachoendlea pale ni uzembe au kuvutana, nakupa miezi mitatu hospitali iwe imemalizika, nifungue wananchi wapate huduma.”

error: Content is protected !!