December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Irine, Edna wahitimu bora UDSM, Rais msaafu Kikwete awapa neno

Spread the love

 

WASICHANA Irine Christopher Msengi, ameibuka kuwa mwanafunzi bora katika shahada ya awali ya Biashara katika Uhasibu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) nchini Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mbali ya Irine, mwanafunzi mwingine bora ni Edna Davis Meela aliyefuzu shahada ya awali ya Sayansi katika Uhandisi Kemikali na Usindikaji yaani (Bachekor of Science in Chemical and Prcessing Engineering).

Irine na Edna, wamefaulu kwa daraja la kwanza kwa Wakia (GPA) wa 4.7 ambao ni ufaulu wa juu kupita wahitimu wote 4,298.

Wawili hao pamoja na wahitimu wengine, walitunukiwa shahada zao jana Jumamosi, tarehe 16 Oktoba 2021 na Mkuu wa chuo hicho ambaye pia ni Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete.

Katika ukurasa wake wa kijamii wa Twitter, Kikwete ameandika “ nimewatunuku shahada za kwanza wanafunzi wapatao 4,298 wa UDSM.

Kati yao, wanawake ni 1,973 sawa na asilimia 45.9. Nilifarijika zaidi kuona katika wahitimu wawili, Bi. Edna Meela na Irene Msengi miongoni mwa walioongoza kwa GPA kubwa.”

error: Content is protected !!