Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Vinara sayansi watengewa Sh bilioni 3
ElimuTangulizi

Vinara sayansi watengewa Sh bilioni 3

Spread the love

SERIKALI kupitia wizara ya elimu, sayansi na teknolojia imetenga kiasi cha Sh bilioni tatu katika mwaka huu wa fedha 2022/2023 kufadhili wanafunzi ambao wamefaulu vizuri masomo ya sayansi katika mitihani inayoandaliwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na kuwasomesha bure hadi ya elimu ya juu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 29 Julai, 2022 jijini Dar es Salaam Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuelezea mwelekeo wa elimu katika mwaka wa fedha 2022/23.

Akifafanua kuhusu ufadhili huo ambao wengi wanataka uitwe ‘Samia Scholarship’, alisema kigezo kimojawapo kwa wanafunzi ambao ni vinara wa masomo ya sayansi ni kuwa tayari kuendelea na masomo ya sayansi, uhandisi au elimu tiba.

“Hizi bilioni tatu ni kwa mwaka huu, mwakani zinaweza kuongezeka kwa sababu hizi za mwaka huu hazikuwepo kwenye bajeti, sisi kama wizara tumejibana kwenye posho na usafiri ndipo tukafanikiwa kupata hizo bilioni tatu ambazo lengo ni kuongeza hamasa ya masomo ya sayansi.

“Pia tutaweka dirisha kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ili nao waweze kunufaika na ufadhili huo ambao utakuwa unatolewa bila kujali huyu katoka wapi au familia gani, ilimradi awe amefaulu vizuri sayansi na afahamu kuwa, anasoma kwa kodi ya Watanzania, hivyo anapaswa kuonesha bidii ili aje kuwahudumia kupitia taaluma yake,” alisema.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

Habari za SiasaTangulizi

Kinana: Hatukubali kushutumiwa kwa uongo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema viongozi wa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

error: Content is protected !!