Wednesday , 17 April 2024
Home Gazeti Habari Serikali kutoa tamko leo nyongeza mishahara
HabariTangulizi

Serikali kutoa tamko leo nyongeza mishahara

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajia kutoa tamko la Serikali kuhusu nyongeza ya mishahara ya watumishi wa umma iliyoanza Julai mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Kwa mujibu wa ukurasa wa twitter wa Msemaji Mkuu wa Serikali, Waziri Mkuu Majaliwa atatoa tamko hilo leo Ijumaa tarehe 29, Julai, 2022 majira ya saa 10.00 jioni.

Tamko hilo linakuja baada ya vikao baina ya Serikali na viongozi wa Shrikisho la vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) yalioanza Jumanne tarehe 26, 2022 ambapo katika kikao cha kwanza pande hizo zilishindwa kufikia mwafaka.

Serikali kupitia Msemaji wake Gerson Msingwa, ilisema viongozi wa TUCTA wameomba kupewa muda wa kujadiliana wenyewe suala hilo na kisha kuendelea na mazungumzo.

Musiba alisema wakishafikia muafaka Serikali itatoa tamko rasmi juu ya suala hilo.

Hata hivyo Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya alisema katika kikao hicho waliionesha Serikali namna ambavyo hawakubaliani na kiwango cha nyongeza ya mishahara na kuitaka kwenda kuangalia upya suala hilo.

Pia aliandaa mapendekezo yao kwa maandishi ambayo Jumatano tarehe 27, Julai, 2022 waliyawasilisha kwa Ofisi wa Waziri Mkuu, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za SiasaTangulizi

Makonda kung’oka tena

Spread the loveUWEZEKANO wa Paul Makonda, kuendelea na wadhifa wake wa mkuu...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu: Mabeyo awataje waliotaka kuzuia urais wa Samia

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu...

Habari za SiasaTangulizi

Vilio vyatawala miili ya wanafunzi wanafunzi ikiagwa Arusha

Spread the loveHUZUNI na vilio vimetawala kwa maelfu  ya waombolezaji wakiwemo familia...

error: Content is protected !!