Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Prof Mushi kuongoza jopo uchambuzi mikopo elimu ya juu
Elimu

Prof Mushi kuongoza jopo uchambuzi mikopo elimu ya juu

Spread the love

SERIKALI imeanza mchakato wa uchambuzi wa mifumo ya utoaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita ili kubaini kasoro zilizopo katika mfumo huo na kutafutia ufumbuzi.

Jopo hilo la wachambuzi wa mifumo ya takwimu kwa njia ya kompyuta, linaongozwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Fedha na Utawala, Profesa Allen Mushi. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea)

Hayo yamebainishwa leo tarehe 29 Julai, 2022 jijini Dar es Salaam Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuelezea mwelekeo wa elimu katika mwaka wa fedha 2022/23.

Akizungumzia mikakati ya wizara hiyo katika utoaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka huu, Prof Mkenda alisema katika bajeti ya wizara hiyo ambayo ni Sh trilioni 1.49 kwa mwaka huu wa fedha, jumla ya Sh bilioni 570 zimetengwa kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu.

Alisema dirisha la uombaji wa mikopo hiyo tayari limefunguliwa lakini pia wizara hiyo imeunda timu iliyoanza kazi ya kufuatilia mifumo ya utoaji mikopo ya elimu ya juu ili kuondokana na malalamiko yanayojitokeza mara kwa mara.

Alisema timu hiyo inaongozwa na watalaam wa ufuatiliaji wa mifumo ya kitakwimu kwa njia ya kompyuta ambao ni Profesa Allan Mushi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Idd Makame kutoka Zanzibar na Dk. Martin Chegelo ambao watafuatilia mifumo ya utoaji wa mikopo hiyo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Alisema ufuatiliaji huo utaimarisha upatikanaji wa taarifa sahihi za waombaji, mathalani waliosomeshwa na wasamaria wema kuanzia shule za awali mpaka kidato cha sita ili waweze kupatiwa mikopo lakini pia wanufaika wa Mpango wa kaya maskini kupitia TASAF nao pia wapatiwe kipaumbele.

MIKOPO UFUNDI

Aidha, alisema kwa wanafunzi wanaojiunga na vyuo vya ufundi kwa kuwa sasa Serikali haijaweka utaratibu wa kuwapatia mikopo lakini Wizara hiyo ilizungumza na Benki ya NMB ambayo imekubali kutenga kiasi cha Sh bilioni 200 ili kuwezesha wanafunzi hao wakope kwa riba nafuu ya asilimia tisa pekee.

Alisema mpango huo unatekelezwa kwa wale wateja wanaopitisha mapato yao kwenye akaunti za benki hiyo kama vile watumishi ambao wanalipwa mishahara kupitia akaunti za benki hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

error: Content is protected !!