Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari Serikali ya Tanzania yaagiza uchunguzi ajali za wanahabari
HabariTangulizi

Serikali ya Tanzania yaagiza uchunguzi ajali za wanahabari

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imeagiza uchunguzi dhidi ya wimbi la wanahabari kupata ajali, wakiwa katika misafara ya viongozi wa umma. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Agizo hilo limetolewa leo Jumatano, tarehe 12 Januari 2022 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, katika shughuli ya kuaga miili ya wanahabari watano, waliopoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea jana Jumanne mkoani Simiyu.

Wanahabari waliopoteza maisha ajalini wakiwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel, ni Abel Ngapemba, Johari Shani, Husna Mlanzi, Steven Msengi na Antony Chuwa.

Miili yao imeagwa katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

“Kumekuwa na matukio ya ajali kwenye misafara mbalimbali ya viongozi wetu na bahati mbaya ajali hizi waathirika wakubwa ni wanahabari.

“Viongozi wangu wameguswa na jambo hili na wameagiza tupitie ajali zote zilizohusisha wanahabari kwenye misafara,” amesema Nape.

Nape amesema “Desemba 2021, ilitokea ajali moja Mtwara, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara alikuwa anakwenda kwenye ziara ikatokea ajali namna hii ikaumiza wanahabari, juzi juzi Julai nadhani alikuwa waziri wa madini yenyewe ikatokea ajali ikahusisha wanahabari. Hii nayo imeondoa wanahabari.”

Waziri huyo wa habari, ameagiza Jeshi la Polisi nchini, liwasilishe ripoti ya ajali zote za barabara zilizohusisha waandishi wa habari, ili kubaini chanzo chake kwa lengo la kutafuta mwarobaini wake.

“Viongozi wangu wameagiza tuombe wenzetu wa Jeshi la Polsii watuletee ripoti ya ajali hizi, tuzipitie tuone kwa nini zinagusa wanahabari na tuchukue hatua ya kuweka itifaki nzuri itakayowalinda wanapotimiza wajibu wao kwenye misafara ya viongozi wetu,” amesema Nape na kuongeza:

“Naahidi tutalisimamia tuhakikishe mnakuwa salama katika kutimiza majukumu yenu, ziko sababu nyingi zinazungumzwa lakini tunataka tujiridhishe kutoka kwenye vyombo vyetu, kuhakikisha kwamba tunazo sababu za kweli kwa nini ajali hizi zinawagusa zaidi wanahabari.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

Habari za SiasaTangulizi

Kinana: Hatukubali kushutumiwa kwa uongo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema viongozi wa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

error: Content is protected !!