Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari Wezi wavunja kanisa, wapika ndizi na kula, waiba vifaa
Habari

Wezi wavunja kanisa, wapika ndizi na kula, waiba vifaa

Spread the love

 

WAUMINI wa Kanisa la Kiadventista la Boigesa lililopo katika eneo Bunge la Bobasi kaunti ya Kisii nchini Kenya, wamepigwa na butwaa siku ya Jumamosi tarehe 8 Januari, mwaka huu baada ya kukuta kanisa lao limevunjwa na watu wanaosadikiwa kuwa wezi. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea)

Kwa mujibu wa Mzee wa Kanisa hilo, Tom Mosoba amesema wezi hao walivunja kanisa hilo usiku wa Jumatano wiki iliyopita, wakapika ndizi, wakala na kuiba vyombo, mfuko mmoja wa mahindi, spika mbili, kipaza sauti na gitaa.

Mosoba aliwaelezea waandishi wa habari kuwa wezi hao walimsukuma mmoja wao kupitia kwenye mwanya uliopo kwenye paani huku wenzake wakitumia shoka kuvunja mlango.

Chifu wa eneo hilo Henry Mirera alisema mshukiwa mmoja wa kisa hicho ambaye ni mkazi wa Kenyenya alikamatwa na sasa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Itumbe kwa mahojiano zaidi.

“Mshukiwa alinaswa katika eneo la tukio kukabidhiwa kwa maofisa wa upelelezi wa makosa ya jinai kwa uchunguzi zaidi,” alisema Mirera.

Aidha, alisema makanisa mengi katika mtaa huo hayana walinzi hivyo wazee wa kanisa wanatakiwa kubeba vyombo vyao vya kanisani na kuvirudisha siku ya ibada ili kupunguza wimbi la uhalifu huo.

Inaelezwa kuwa tukio hilo, limejiri siku chache baada ya wezi wengine kuvamia kanisa moja Kaunti ya Vihiga nchini humo na kupaka kinyesi kuta za kanisa hilo.

Wakazi mtaa huo waliachwa na mshtuko baada ya watu wasiojulikana kuvamia Kanisa la Mumbita Church of God Luanda na kuacha haja kubwa ndani ya ofisi ya mchungaji.

Tukio hilo limelazimisha uongozi wa Kanisa hilo Church of GOD Afrika Mashariki nchini Kenya kuandaa sherehe ya utakaso ili kufukuza pepo na kuweka wakfu tena wa kanisa la Mumbita.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa ustawi wa jamii katika mkutano mkuu wa kanisa hilo, Wycliffe Ochieng wezi hao pia waliiba lita 40 za rangi zilizokuwa zimehifadhiwa ndani ya kanisa hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariHabari Mchanganyiko

CRB yashtukia makandarasi wanaofanya ubia wa ujanja ujanja, yasema watakaobainika kuchukuliwa hatua kali

Spread the love  BODI ya Usajili wa Makandarasi (CRB), imeonya makandarasi wanaofanya...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Habari

Mnyika aacha ujumbe msibani kwa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Taifa, John...

HabariHabari Mchanganyiko

Mwili wa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine wawasili, kuzikwa Mbeya

Spread the loveMWILI wa Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, aliyefia...

error: Content is protected !!