Spread the love

 

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umesema kama nchi ingekuwa na katiba nzuri, changamoto  ya mgawanyo wa madaraka isingekuwepo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kauli hiyo ilitolewa leo , tarehe 11 Januari 2022 na Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa,  akimjibu Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, aliyesema nguvu ya Rais haiwezi kulingana na viongozi wa mihimili  mingine.

“Na tufahamu kwamba,  bado Tanzania  hatujafikia level (ngazi) ya full separation of power (mgawanyo wa madaraka),  bado tuna changamoto ya mfumo wa mgawanyo wa  madaraka ukilinganisha na nchi nyingine.  Mfumo wetu  wa kiuongozi bado haujaweza kuweka mipaka kamili baina ya mihimili mitatu ya kitaifa,” amesema Olengurumwa.

Olengurumwa almesema  “hoja ibakie mihimili yetu hii inapaswa kuwa huru na haipaswi kuingiliana, kila mmoja afanye kazi kwa majukumu yake. Kwa sababu katiba ndiyo imeweka hivyo,  Bunge linaweza kumuondoa Rais na Rais kulivunja Bunge,  lakini pia mahakama ingekuwa tuna katiba nzuri kama ya Kenya,  inauwezo  wa kufanya maamuzi makubwa dhidi ya Bunge na Serikali.”

Mratibu huyo wa THRDC, amesema dhana ya mgawanyo wa madaraka iliwekwa ili kuondoa nguvu ya madaraka ya kuongoza nchi kwa mtu mmoja.

“Dhana ya mgawanyo wa madaraka ni dhana ambayo iliwekwa toka karne ya 16 wakati mifumo ya utawala wa mabwanyeye imeshika kasi,  hoja yao kubwa ilikuwa tuondoe madaraka kwa mtu mmoja lengo kuondoa mazingira ambayo kutakuwa na matumizi mabaya ya madaraka katika mataifa yetu,” amesema Olengurumwa.

Akijibu kauli ya Dk. Tulia aliyotoa hivi karibuni, Olengurumwa amesema “hoja ya Dk. Tulia imebezi zaidi kwenye masuala ya equality of power  (usawa wa madaraka),  kitu ambacho hatuna hiyo hoja na hakuna mtu anayeweza simama akalinganisha Rais na mahakamavna Bunge,  sababu taasisi zote hizi ni za kikatiba na katiba imetoa taasisi hizi kwa lengo la kugawanya madaraka ili kuepuka taasisi moja kuonekana iko juu ya nyingine.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *