Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari Lissu atuma ujumbe Ikulu
HabariTangulizi

Lissu atuma ujumbe Ikulu

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Chadema
Spread the love

TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)- Bara, amemshauri Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kufanya mabadilio ya sheria. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kiongozi huyo wa Chadema ambaye alikuwa mgombea urasi wa chama hicho katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana, na kushika nafasi ya pili amesema, maneno matamu ya Rais Samia yaende sambamba na mabadiliko ya sehria.

Ujumbe wa Lissu, ameueleza kupitia ukurasa wake wa twitter jana tarehe 6 Aprili 2021, akizungumzia kauli ya Rais Samia kuhusu utendaji kazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kwenye ukurasa huo, Lissu ameandika “maneno matamu tu hayatoshi. Kinachohitajika ni mabadiliko makubwa ya sheria za kodi na TRA ili kuweka Taxpayers Bill of Rights (haki za walipa kodi) na uwajibikaji kwa serikali na wakusanya kodi wake…”

Kwenye andiko hilo, Lissu ambaye aliwahi kuwa Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), ameeleza, kama sheria hazitabadilika kile alichoita dhulma dhidi ya walipa kodi na rushwa za wakusanya kodi, hazitaisha.

Jana Jumanne, akizungumza wakati akiwaapisha makatibu, manaibu makatibu na viongozi wa taasisi za serikali, Rais Samia alisisitiza matumizi ya akili zaidi kwa TRA kuliko nguvu kwa wafanyabiashara.

Kuongozi huyo alisema, matumizi ya nguvu na kukandamiza wafanyabiashara kunaua biashara, na kwamba biasha zikifa TRA itashindwa kupata kodi.

Samia Suluhu Hassani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

“Wito wangu kwa TRA, matumizi ya ubabe na maguvu katika ukusanyaji mapato, haisaidi. Inasaidia kwa muda mfupi, nimepwa takwimu za Task Force (kikosi kazi) zenu mnavyoziunda na jinsi mnavyokusanya, lakini haiko sustainable (imara).

“Sababu mtakwenda mtambinya mtu, mtakumkamua mtakusanya leo kiasi mlichotaka, mtapiga kesi za uhujumu uchumi ataogopa kwenda jela atajikwangua atalipa, lakini unaua biashara yake. Kesho na keshokutwa nani anakulipa kodi” alihoji Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

Habari za SiasaTangulizi

Kinana: Hatukubali kushutumiwa kwa uongo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema viongozi wa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

error: Content is protected !!