Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari Vita dawa za kulevya: IGP Sirro atoa maagizo
Habari

Vita dawa za kulevya: IGP Sirro atoa maagizo

Spread the love

 

INSPEKTA Jenerali wa Polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirro, ameagiza makamanda wa jeshi hilo hasa katika Mikoa ya Mtwara, Lindi, Tanga, Dar es Salaam, Unguja na Pemba, wadhibiti mtandao sugu wa dawa za kulevya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

IGP Sirro ametoa agizo hilo hivi karibuni wakati anazungumzia hali ya usalama nchini katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi 2021.

Aliwaagiza makamanda hao kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, kutokomeza biashara ya dawa za kulevya.

“Kuna shida ya dawa za kulevya, lakini kamanda wa mikoa ya Mtwara, Lindi, Tanga, Dar es Salaam, Pemba na Unguja, lazima mfanye operesheni za pamoja, hili suala haliwezi kutushinda. Uwezo mkubwa tunao kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama,” alisema IGP Sirro.

Mbali na kudhibiti mtandao wa dawa za kulevya, IGP Sirro aliwaagiza makamnda wote wa Jeshi la Polisi, kutokomeza vitendo vya udhalilishaji.

Baadhi ya dawa za kulevya

“Sasa yamebakia makosa ya udhalilishaji na madawa ya kuleva, lazima ifike mahala tuseme basi, na wale ambao ni sugu sisi tuwe sugu zaidi, sheria zipo tuhakikishe tunaisimamia na hao wanatiwa hatiani,” aliagiza IGP Sirro.

Akizungumzia hali ya usalama nchini, IGP Sirro alisema makosa ya jinai yamepungua kwa asilimia 19.1 wakati ya usalama barabarani yakipungua kwa asilimia 14.

“Ukiona kwa miezi mitatu makosa ya jinai yamepungua kwa asilimia 19.1 sio jambo dogo, lakini ukiwa na makosa ya usalama barabarani yamepungua kwa asilimia takribani 14 si jambo dogo, kwa hiyo kuna kazi inafanyika,” alisema IGP Sirro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!