Tuesday , 30 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Milioni 9 waambukizwa corona duniani
Kimataifa

Milioni 9 waambukizwa corona duniani

Spread the love

MAAMBUKIZO ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) duniani, yamefikia milioni 9.19 huku waliopona wakiwa milioni 4.94. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa mtandao wa ‘worldometer’ leo Jumanne tarehe 23 Juni 2020 unaonyesha vifo vinavyotokana na ugonjwa huo vimefikia 474,479.

Marekani ni Taifa linaloongoza kwa maambukizo mengi ya watu milioni 2.38, waliopona wakiwa milioni moja huku vifo vikiwa  122,611.

Brazil ina wagonjwa milioni 1.1, vifo 51,407 huku waliopona ugonjwa huo wakiwa 594,104.

China ambako ugonjwa huo ulianzia mwishoni mwa mwaka 2019, kuna wagonjwa 83,418, waliofariki dunia wakiwa 4,634 na waliopona ni 78,425.

Nchini Kenya, maambukizo yamefikia 4,797, waliopona 1,680, waliofariki dunia wakiwa 125 huku idadi ya sampuli zilizokwisha kupimwa ni 142,366

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!