Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Majaji kuamua hatima ya Zuma leo
Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the love

Majaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa zamani wa nchi hiyo, Jacob Zuma ataruhusiwa kugombea kwenye uchaguzi wa Mei mwaka huu. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Zuma ambaye anawania kwa tiketi ya chama cha upinzani, alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa maafisa wa tume ya uchaguzi waliomkatalia kugombea kutokana na kupatikana na hatia mwaka 2021.

Jana Jumatatu, Zuma mwenye umri wa miaka 81 alikuwa mahakamani mjini Johannesburg wakati mawakili wakijadi kesi hiyo.

“Ikiwa raia wanataka niwe rais, nani atawazuia?”, Zuma aliwambia wafuasi wake baada ya kesi kusikilizwa. “Niruhusu niende na nimalizie kile nilichokianza.”

Afrika Kusini inafanya uchaguzi mkuu tarehe 29 Mei ambao unatarajiwa kuwa uchaguzi wenye ushindani mkali tangu ujio wa demokrasia mwaka 1994.

Chama tawala cha African National Congress kinakabiliwa na changamoto katika kura ya maoni na kuna hatari kipoteza wingi wa wabunge tangu kumalizika kwa utawala wa kibaguzi, kutokana na uchumi dhaifu na madai ya ufisadi na usimamizi mbaya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni

Spread the loveAliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Peter...

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

error: Content is protected !!