Tuesday , 30 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan
Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the love

Watu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800 wamejeruhiwa baada ya tetemeko kubwa la ardhi kuikumba nchi ya Taiwan leo Jumatano asubuhi na kusababisha uharibifu mkubwa wa majengo, miundombinu na barabara. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa… (endelea)

Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Taiwan (CWA) imesema kuwa tetemeko hilo la ardhi lilikuwa na ukubwa wa 7.4 katika kipimo cha Richter, huku Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani, USGS likisema chimbuko la tetemeko hilo ni kilomita 18 kusini mashariki mwa kaunti ya Hualien, katika kina cha kilomita 34.8.

Idara ya Kitaifa ya Zimamoto na uokoaji nchini humo imeeleza kuwa takribani majengo 26 yameanguka, huku zaidi ya nusu ya idadi hiyo yakiporomoka kwenye kaunti ya mashariki ya Hualien.

Pia idara hiyo imesema vifo vyote vimetokea katika kaunti hiyo, na kwamba hadi sasa watu 820 wamejeruhiwa.

Aidha, ripoti zinaeleza kuwa waokoaji wanatumia ngazi kuwaokoa watu na kuwapeleka maeneo salama.

Picha na video zilizorushwa kwenye televisheni za Taiwan zimeonyesha maghorofa mengi kwenye kaunti ya Hualien na kwengineko yakiporomoka na kutitia na mengine yakiwa yamepinda, huku ghala katika jiji la Taipei likiwa limebomoka.

Meya wa Taipei amesema zaidi ya watu 50 walionusurika walifanikiwa kuokolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo hilo.

Mmoja wa wakaazi wa Taipei, Fu Zhong Mei, amesema ”Nilipogungua kuwa ni tetemeko, haraka nilivaa nguo na viatu, kisha nikamchukua mwanangu tukakimbia na kushuka ngazi. Sijachukua kitu chochote,” alifafanua Fu.

Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Matetemeko cha Taipei, Wu Chien-fu amesema tetemeko hilo limesikika kote nchini Taiwan na kwenye visiwa vya pwani.

Wu amesema umma unapaswa kuzingatia tahadhari na ujumbe unaootolewa na watu wanapaswa kuwa tayari kuondolewa kwenye makazi yao kutokana na tetemeko hilo la ardhi.

Watu wengine 60 wamekwama kwenye njia za chini ya ardhi ya Jinwen, barabara kuu ambayo inaiunganisha miji ya Suao na Hualien.

Wu amewaambia waandishi habari kuwa tetemeko hilo la ardhi ni kubwa kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 25 iliyopita.

Kwa mujibu wa Wu, tetemeko la mwisho lenye ukubwa wa 7.6 katika kipimo cha Richter, lilitokea Septemba 1999, na kuwaua watu wapatao 2,400, hayo yakiwa ni majanga mabaya zaidi ya asili katika historia ya kisiwa hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Habari Mchanganyiko

TMA yapongezwa kuimarisha ubora na usahihi wa taarifa za Hali ya Hewa

Spread the love  WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

error: Content is protected !!