Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bil 12.4 zimetumika ujenzi wa miradi wilaya ya Momba
Habari Mchanganyiko

Bil 12.4 zimetumika ujenzi wa miradi wilaya ya Momba

Spread the love

MKUU wa wilaya ya Momba mkoani Songwe Kennan Kihongosi ame tumia sherehe za  siku ya Muungano wa Tanganyika kutaja mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Dk. Samia Suruhu akisema alitoa Bilioni 124 zilizojenga miradi. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe … (endelea). 

Amesema serikali ya awamu ya sita inafanya kazi kubwa ya kuwa ondolea wananchi changamoto zinazowakumba hivyo kazi iliyopo ni kuhakikisha miradi inatunza ili iweze kusaidia hadi vizazi vijavyo kwa ni amegusa kila sekta ikiwemo elimu, afya, maji, miundo mbinu na nishati.

DC Kihongosi aliyasema hayo tarehe 26 Aprili, 2024 wakati wa maadhi misho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania na Zanzibar yaliyofanyika kijiji na kata ya Kamsamba wilayani Momba mkoani humo.

Amesema kwenye elimu zimetumika, Sh. 31 bilioni, afya Sh. 14.4 bilioni, vifaa tiba Sh. 1.6 bilioni, Maji Sh. 17.8 bilioni huku vitongoji 142 vikiwekewa umeme ambapo vitongoji 153 kazi inaendelea na pia Sh. 6 bilioni zikitumika ujenzi wa barabara, makalavati na madaraja ndani ya miaka mitatu.

Amesema katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2024 cha utawala wake wa miaka mitaatu ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, wilaya ya Momba ilipokea Tsh,124,062,121,574.23 ikiwa ni kiasi cha Tsh, 45,499,583,419.41 zilienda halmashauri ya mji Tunduma na Tsh, 31,870,007,687.56 zilienda halmashauri ya Momba.

Ameongeza kuwa katika sekta ya kilimo mifugo, wameweza kujenga miradi ya kimkakati, soko la kimataifa la mazao na mifugo kakozi,(Maghara ya kuhifadhia mazao), jengo la kuuzia mazao, mnada wa mifugo na jengo la machinjio na pia pikipiki 23 zilinunuliwa kwa ajili ya maafisa kilimo zikiwemo 8 zilizonunuliwa kwa fedha za mapato ya ndani.

Ameongeza kuwa ujenzi wa majosho sita ya kuogeshea mifugo imeje ngwa kwenye vijiji vya Chitete, Msangano, Nzoka, Ivuna, Mkulwe na Mkomba huku ununuzi na usambazaji wa mbegu za ufuta kwa waku lima ukifanyika kuwaongezea tija na hamasa ya stakabadhi ghala ni ikiwemo ununuzi wa chanjo za mifugo.

Ameeleza kuwa Kiasi cha Tsh,1,974,892,771.14 kilitumika kwa ajili ya sensa ya watu na makazi ya 2022 ambapo wilaya ya Momba yenye wakazi 551,090 na kaya 114,687 ambapo halmashauri ya Momba yenye wakazi 259,781 na kaya 58,098 na halmashauri ya Tunduma ina wakazi 291309 na kaya 56,589.

‘’Leo ni kilele cha Muungano ambapo waasisi wa nchi hii mahayati Mwalimu Julias Nyerere na Abed Kalume mwaka 1964 walikubaliana Zanzibar na Tanganyika kuuungana,hivyo kuna kila sababu ya kuimarisha na kuulinda muungano huo na tayari tumeona maendeleo mengi yakifanyika.

Naye Shekhe Mkuu mkoani wa Songwe, Husein Batuza amesema wao kama viongozi wa dini wana kila sababu ya kuliombea Taifa na viongozi wake huku akimsifu Rais Dk. Samia kwa kupeleka fedha nyingi mkoani Songwe zilizojenga miradi ya maendeleo inayogusa jamii.

Diwani mwenyeji Chalambwenge Kakwale, katika maadhimisho hayo mbali na kuipongeza serikali kupeleka fedha nyingi za miradi iliyoje ngwa hata kwenye kata yake,lakini alitumia nafasi hiyo kutoa kero za ukosefu wa X-ray mashine kwenye kituo cha afya Kamsamba ambapo mkuu wa wilaya ameahidi kuifanyia kazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile aukwaa uenyekiti wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!