Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Trump aita corona ‘kung flu’
Kimataifa

Trump aita corona ‘kung flu’

Spread the love

KAULI ya Donald Trump, Rais wa Marekani kuita virusi vya corona (COVID-19), ‘kung flu’ imetetewa na msemaji wa Ikulu nchini humo. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Akizungumza Tulsa, Oklahoma mwishoni mwa wiki, Trump alisema virusi hivyo vilivyoanzia Wuhan, China vina majina mengi kuliko ugonjwa wowote kwenye historia ya magonjwa ya mlipuko.

 “Unaweza kuita ‘kung flu,’” Trump alisema wakati wa mkutano huo na kuongeza “naweza kuita ugonjwa huu majina 19 tofauti.”

Kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, msemaji wa Ikulu, Kayleigh McEnany amesisitiza, kauli ya Tump inaweka rekodi sawa kwamba ugonjwa huo umetokea China.

“Chanzo cha virusi vya corona ni China, ni haki kabisa kueleza hivyo, China inajaribu kuficha historia hiyo, ilitaka kuaminisha kuwa virusi hivyo walikuwa navyo wanajeshi wa Marekani. Ndio! Rais Trump alisema ‘nitataja virusi hivi kwa jina halisi la eneo vilipotokea,’” amesema McEnany.

McEnany alitakiwa kutoa ufafanuzi kutoka kwa mwandishi Mmarekani mwenye asili ya Asia, ambaye alionekana kutofurahishwa na kauli ya Trump.

“Rais alisema wazi, kwamba ni jambo la msingi kulinda Wamarekani wenye asili ya Asia na kokote kule duniani,” alisema mwandishi huyo.

McEnany alijibu “sio suala la mjadala hilo, wote hao rais anajua kuwa ni raia na wana haki kama Wamarekani,” ameongeza “lakini ni uhalisia kwamba China ndio walioingiza ugonjwa huo hapa nchini.”

Katika maelezo yake, McEnany badala ya kusema corona alitamka ‘Wuhan virus’ akimaanisha COVID-19 huku akishutumu vyombo vya habari kutumia maneno tofauti na hayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!